MKUU wa wilaya ya Morogoro Mhe. Adv. Albert Msando , ameongoza zoezi la ugawaji vishikwambi 1259 kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari zilizopo Manispaa ya Morogoro.
Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro Januari 19/2023.
Akizungumza katika zoezi hilo , DC Msando, amewataka walimu kutunza zana hizo za kazi (vishikwambi) pamoja na kufuata maelekezo yote yaliyotolewa kutoka kwenye muongozo juu ya utunzaji na utumiaji.
“Tunakila sababu ya kuishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuboreshea miundombinu katika sekta ya elimu, nendeni mkavitumie vishikwambi (tablet) hivi kwa malengo yaliyokusudiwa, tumieni vishikwambi hivi katika mambo ya msingi kama kutumiana maswali, kapakua vitu mbalimbali vya ufundishaji mtandaoni lengo ni kuongeza ufaulu katika shule za Msingi na Sekondari. " Amesema DC Msando.
Aidha, amesema, vishikwambi hivyo vimeletwa kwa kwa ajili ya matumizi ya kujifunzia na kufundishia kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari na sio kwa matumizi mengine ,hivyo amewataka waalimu wakatekeleze utumiaji wa zana hizo kama masharti yalivyoelekezwa katika muungozo wa matumizi yake.
Naye Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Morogoro , Gabriel Paul, amesema kuwa upande wa Elimu Msingi jumla ya vishikwambi 893 vimegaiwa na upande wa Shule za Sekondari vimegaiwa vishkwambi 366.
" Niwaombe Waalimu kuzingatia usalama katika utunzaji wa vishikwambi hivyo na nitoe wito kwa waalimu wote waliopata vishikwambi hivyo waweze kushirikiana na wengine ambao hawajapata ili waendelee kuboresha ujifunzaji na ufundishaji shuleni" Amesema Gabriel.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa