MANISPAA ya Morogoro imepokea kiasi cha Bilioni 1,401,200,000.00 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa BOOST kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule kumi (10) za Msingi.
Akizungumza mara baada ya kupokea fedha hizo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amesema , Boost ni sehemu ya Mpango wa Lipa kulingana na Matokeo katika elimu awamu ya pili (EPforRII) na inachangia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu wa miaka mitano 2020/2021 hadi 2025/2026.
"Tunaishukuru Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupokea kiasi hiki kikubwa cha fedha, mradi huu wa Boost utasaidia katika ujenzi wa miundombinu kama vile madarasa na vyoo pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu ili kuwaongezea uwezo wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule zao pamoja na kuboresha upatikanaji fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi." Amesema Machela.
Miongoni mwa shule zinazonufaika na mradi wa Boost ni Shule ya Msingi Muungano Kata ya Mafisa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa yenye thamani ya milioni 66,000,000.00 na , shilingi milioni 5,400,000.00 ujenzi wa matundu 3 ya vyoo, Shule ya Msingi Nanenane Kata ya Tungi ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa yenye thamani ya milioni 66,000,000.00 na shilingi milioni 5,400,000.00 ujenzi wa matundu 3 ya vyoo, Shule ya Msingi Mgolole ujenzi wa madarasa 2 milioni 60,800,000.00, Shule ya Msingi Mazimbu A darasa 1 milioni 22,000,000.00 na matundu 3 ya vyoo milioni 5,400,000.00, Shule ya Msingi Kingolwira vyumba 3 vya madarasa milioni 66,000,000.00 na matundu 3 ya vyoo milioni 5,4000,000.00, Shule Msingi Kilongo Mkundi madarasa 3 milioni 66,000,000.00 na matundu 3 ya vyoo milioni 5,4000,000.00,Shule Msingi Kambarage Chamwino madarasa 2 milioni 44,000,000.00 na matundu 3 ya vyoo milioni 5,4000,000.00, Shule Msingi Jitegemee Chamwino ujenzi wa shule mpya milioni 475,300,000.00, Shule Msigi Bungo Boma darasa 1 milioni 22,000,000.00 na matundu 3 ya vyoo milioni 5,4000,000.00, pamoja na Shule Msingi Kihonda Maghorofani ujenzi wa shule mpya milioni 475,300,000.00.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa