HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepokea jumla ya kiasi cha shilingi Bilioni1.8 ya fedha za ruzuku kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, fedha za matumizi ya kawaida na fedha za elimu bure bila malipo.
Akizungumza juu ya mapokezi ya fedha hizo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amesema fedha hizo zimetolewa kwa mwezi Septemba kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya kidato cha kwanza 2023.
Machela,amesema kuwa fedha hizo zimetolewa kupitia mpango wa elimu bure bila malipo kwa shule za Msingi na Sekondari na fedha za matumizi ya kawaida (OC).
" Tunamshukuru sana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha hizi ambazo zitakuwa mkombozi kwa watoto wetu, na tutazitumia vizuri kwa kuzingatia thamani ya fedha katika madarasa ambayo tutayajenga" Amesema Machela.
Mchanganuo wa fedha hizo ni kwamba Tsh. Milioni 1,620,000,000.00 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha kwanza 2023, Tsh milioni 209,379,241.00 zitatumika kwa ajili ya elimu bila malipo kwa shule za Msingi na Sekondari na Tsh. Milioni 40,736,00.00 zitatumika kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Hii ni mara ya pili kupokea fedha ,ikumbukwe Manispaa ilipatiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 86 ya Uviko 19.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa