HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepokea Ruzuku kutoka serikali kuu jumla ya shilingi 620,014,716.00 kwa mwezi April 2023.
Akizungumza Juu ya mapokezi hayo ya fedha hizo za Ruzuku, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Ally Machela, ameishukuru Serikali kwa kuipatia Manispaa fedha za Ruzuku na kuahidi kuzitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Machela amefafanua mchanganuo wa fedha hizo kama ifuatavyo ambapo Tsh.40,736,000.00 kwa matumizi ya kawaida,Tsh 133,038,074.00 kwa matumizi ya Elimu bila malipo Sekondari, Tsh 86,901,203.00 kwa matumizi ya Elimu bila malipo ya Msingi,Tsh.119,770,000.00 kwa matumizi ya Mitihani ya kidato cha sita,Tsh.128,319,439.00 kwa matumizi ya Basket fund robo ya tatu,Tsh.81,250,000.00 kwa matumizi ya Ujenzi wa madarasa shule za msingi na Tsh,30,000,000.00 kwa matumizi ya Ujenzi wa uzio shule maalum.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa