Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro imetoa fedha kwaajili ya mikopo yenye jumla ya milioni 91,000,00 kwa vikundi vya vijana 31.Hayo yamebaishwa na Mkuu wa Wilaya Bi Regina Chonjo wakati wa kugawa hundi kwa vikundi hivyo.
Mhe Chonjo ameeleza kuwa Manispaa ya Morogoro hutenga 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wanawake na vijana na watu wenye mahitaji maalumu,ambapo asilimia 4 ni kwa vikundi vya wanawake na asilimia 4 ni kwa vikundi vya vijana na asilimia 2 ni kwa watu wenye mahitaji maalumu.Riba ya mikopo unaotolewa ni asilimia 10%.
Akizungumza wakati wa halfa hiyo Mhe Chonjo amesema lengo la mfuko wa maendeleo ya wanawake na vijana ni kutoa fursa kwa jamii hivyo ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu.Mikopo hii utolewa ili kuwaongezea mitaji kwenye biashara ambazo tayari zimeanzishwa ili kuwawezesha kujiendeleza kiuchumi na hivyo kuinua hali za maisha.
"Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 Manispaa ilitenga kiasi cha shillingi 342,659,552 kwaajili ya kuvikopesha vikundi vya vijana"alisema Chonjo.
"Vikundi vinavyopewa mikopo ni vile ambavyo vimependekezwa na kamati za maendeleo za kata na kufanyiwa uhakiki na kuonekana vimekidhi vigezo na vikundi vinavyofanya shughuli za viwanda vidogovidogo vimepewa kipaumbele".aliongeza kusema Chonjo
Mkuu uyo wa Wilaya amewasisitiza vijana waliopatiwa mikopo kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwaagiza watendaji wa kata na maafisa Maendeleo ya jamii kusimamia vikundi na kuelewa fedha iliyotolewa ni kodi za wananchi hivyo zinapaswa zitumike na kurejeshwa ili vikundi vingine navyo viweze kukopeshwa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa