Manispaa ya Morogoro kupitia Ustawi wa Jamii imetoa msaada wa magongo 5 kwa ajili ya kuwasaidia baadhi ya Wazee wenye ulemavu walioko kwenye mazingira magumu.
Tukio hilo la kukabidhi vifaa hivyo limefanyika leo Machi 30/2021 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa walengwa, Afisa Ustawi na Mratibu wa Wazee Manispaa ya Morogoro, Rehema Malimi,amesema kuwa Manispaa itaendelea kushirikiana na Wazee pamoja na watu wenye uhitaji maalum ili kuendelea kuwapatia huduma kadri inavyowezekana.
Malimi, amesema kuwa kutolewa kwa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa idara yao ya ustawi wa jamii.
“ Natoa shukrani kwa Mkurugenzi wetu wa Manispaa ya Morogoro kuwa mstari wa mbele katika kuona ustawi wa jamii unasimama na kwa kuweza kuwa bega kwa bega na sisi lakini nitoe pongezi kwa ushirikiano na taasisi mbali mbali katika kuyahudumia makundi maalumu kwani, serikali inaamini kuwa binadamu wote ni sawa bila kujali huyu ana ulemavu au mzee.Tutaendelea kuhakikisha watu wote wanaishi kwa amani”,Amesema Malimi.
Mwisho, Malimi, amechukua nafasi ya kuwaomba wadau wengine kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji katika jamii ili kuendelea na utekelezaji wa shughuli zao za kijamii .
Akizungumza kwa niaba ya Wazee wenye ulemavu ambaye jina lake limehifadhiwa mara baada ya kukabidhiwa magongo hayo, ameishukuru Manispaa ya Morogoro chini ya kitengo cha Ustawi wa Jamii kwa kuona umuhimu wa kuyafikia makundi maalumu ambayo kimsingi yanashiriki katika shughuli za maendeleo katika jamii.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa