HALMASHAURI yaManispaa ya Morogoro imewapongeza wadau mbalimbali wanaoendelea kusaidia Vituo vya Watoto yatima katika kuhakikisha wanapata huduma stahiki.
Kauli hiyo imetolewana Afisa Maendeleo ya Jamii, Mwanitu Sembogo, akimwakilisha Mkurugenzi waManispaa ya Morogoro katika sherehe iliyoandaliwa na Makao ya kuleleaWatoto ya Mgolole ya kumkumbuka Mtakatifu Vicent kwa ajili ya matendoyake aliyokuwa akiyafanya katika kuwasaidia Watoto yatima, Wazee na watuwasiojiweza wenye mahitaji maalumu.
Akizungumza naWaandishi wa habari, Sembogo, ameiomba jamii kuendelea kuelekeza macho katikakusaidia Vituo kama hivyo ili kuvipa uwezo wa kulea Watoto na kupunguza Watotowanaoteseka kwa kukosa msaada.
"Tunashukuru sana Uongozi wa Mgolole kwa hatua mliyofikia licha ya kuwepo kwachangamoto zinazowakabili lakini kiukweli mmekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii, mnatusaidia sana Serikali katika kupunuza wimbi la Watoto mitaani, lakini hiimisaada yote mnayoiona leo hapa kutoka kwa wadau mbalimbali wanatoa iliwatoto hawa nao wajione kama sehemu ya jamii na waweze kutimiza ndoto zaoikiwemo za kupata elimu bila vikwazo pamoja na kusihi kwa matumaini kamawanavyoishi watoto wengine mitaani wakiwa na Wazazi na walezi wao, niwaombewadau tuendelee kumulika kwa jicho pana Vituo vyetu hivi ili tuzuie wimbi laWatoto mitaani "Amesema Sembogo.
Amesema kuwani vema wanajamii wakaendelea kujitolea kwa watoto kama hao ambaowanahitaji msaada wakati wote ukizingatia kuwa hawana wazazi isipokuwa wazaziwao ni jamii inayowazunguka.
Aidha, amesemaManispaa ya Morogoro itaendelea kutoa ushirikiano na Vituo vya kulelea Watotoyatima katika kuhakikisha kwamba Watoto hao wanapatiwa huduma nzuri hukuakitoa pongezikwa mlezi wa kituo hicho na kumshukuru kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao na malezi kwa ujumla.
Mwishoamesema ni vizuri kwa jamii ikajiwekea utaratibu kuwafikia watotohao na wengine wenye hali kama hii na kuwasaidia kwa kadiri itakavyowezakanaili nao hapo baadae waweze kushiriki katika ujenzi wa Taifa katika sektambalimbali kama watumishi na wataalamu.
Naye Mkuu wa Kituo cha Watoto yatima Mgolole, Bi. Maria EvaristaBunga, amewashukuru wageni wote kwa ujio huo na kwa vitu ambavyowamevitoa kwa watoto hao ambao ni yatima ambao wanahitajikufarijiwa.
"Hakika mmesaidia kwa mchango mkubwa na niwakaribishe mara kwa mara kuja kuwatembelea na kuona maendeleo yawatoto hawa.""Amesema Bi. Bunga.
Katika hatua nyengine, mmoja wa wananchi waliofika katikaSherehe hiyo, Marco Kanga, ameshauri kuwa katika kuhakikisha watoto haowanakuwa na afya nzuri ni vyema Serikali na wadau wengine wakachukua jitihadaza makusudi za kuwakatia Watoto hao bima ili ziweze kuwasaidia kupata matibabu.
Mgolole ni miongoni mwa Vituo vya Kulelea Watoto yatima ambapokilianzishwa mwaka 1937 na Baba Askofu Bernard Hilhorst Holanzi ambaye ndiyealikuwa Askofu wa Jimbo la Katoliki la Morogoro na mwakilishi wa Shirika laMasista wa Moyo safi wa Maria wea Morogoro ambao ndio walezi wakuu wa Watotoyatima.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa