Maonesho ya Kanda ya Mashariki yameanza leo Agosti 1,2022 katika Viwanja vya Mwl.Julius K.Nyerere ambayo inashirikisha Mkoa wa Morogoro,Dar es salaam,Pwani na Tanga yenye Kauli mbiu isemayo "Agenda 10/30 kilimo ni biashara,Shiriki kuhesabiwa kwa Mipango bora ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi".
Viongozi mbalimbali wametembelea maonesho hayo kuangalia jinsi gani wajasiriamali wanavyofaidika na kujinyanyua kiuchumi.
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kipekee kabisa inashiriki maonesho haya kwa kuwawezesha wakulima,wafugaji na wajasiriamali wanaonufaika na mkopo wa Asilimia 10 kuweza kuja kuonesha shughuli mbalimbali wanazofanya,lengo ikiwa ni kutoa elimu na kujifunza kutoka kwa wengine.
Akizungumza Afisa Kilimo wa Manispaa Ndg.Michael Waluse amesema maonesho ya haya yameanza rasmi tarehe 1/8/2022.
Waluse ametoa elimu mbalimbali kwa wakulima na kuwaonesha wananchi umuhimu wa kilimo kama msemo usemao Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu.
Pi amewashukuru wakulima wote waliojitokeza kuja kuonesha mazao yao na kutoa Elimu kwa wananchi hasa katika zao la Uyoga.
Mwisho,Waluse amewakaribisha wananchi wote kujitokeza kushiriki Sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 23/2022
"SENSA KWA MAENDELEO,JIANDAE KUHESABIWA".
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa