Jumla ya Miradi 5 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 ikiwa ni utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikishirikiana na Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo.
Thamani ya miradi yote iliyopitiwa na Mwenge ni Tsh. Bilioni 48,689,845,342.22 ambapo Serikali Kuu imetoa Tsh Bilioni 8,066,006,951.22, Manispaa ya Morogoro Tsh Milioni 659,178,280 Wahisani Tsh Bilioni 39,964,526,111 na Wananchi wamechangia Tsh 134,000.
Katika Miradi hiyo Mwenge wa Uhuru umekagua na kuona maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko kuu na kiwanda cha kuchakata mpunga,umewekea jiwe la msingi ujenzi wa jengo la maktaba na utawala shule ya Sekondari Mafiga,umezindua kiwanda cha kutengeneza machujio ya maji na umefungua wodi ya wazazi kituo cha afya Sabasaba.
Akitoa Ujumbe wa Mwenge Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ali aliwasisitiza Wananchi Kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwezi Ockoba 2019 na kueleza ujumbe wa Mwenge ambao ni "Maji ni Haki ya Kila mtu,Tutunze Vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa".
Aidha aliendelea Kuhamasisha wananchi kuhusu Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya Madawa ya Kulevya na Mapambano dhidi ya Malaria.
Aidha alisisitiza kwa viongozi wa serikali kufuatilia kwa makini miradi inayojengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ijengwe kwa ubora unaotakiwa ili thamani ya pesa inayotumika ionekane “Watumishi wote mnatakiwa kutimiza wajibu wenu katika kulitumikia Taifa letu”alisema Mzee
Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 Uliwashwa Rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na alitoa rai kwa Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutumia mbio za Mwenge wa Uhuru kumkumbuka Baba wa Taifa kwa kupinga vitendo vya dhulma, ufisadi, rushwa, maradhi, chuki, dharau na kuwataka kuenzi umoja na mshikamano wetu kuchapakazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa