MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaaziz Abood, amekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 28 kwa Zahanati 5 na Kituo cha Afya kimoja Manispaa ya Morogoro kupitia fedha zake binafsi na fedha za Mfuko wa Jimbo.
Ugawaji waVifaaTiba umefanyika Mei 08-2024 kwenye Zahanati 5 na Kituo cha Afya 1 ikiwemo Zahanati yaTowero na Mbete zote zikiwa Kata ya Mlimani , Zahanati ya Uwanja waTaifa, Zahanati ya Konga Kata ya Mzinga, Zahanati ya Kibwe Kata ya Boma na Kituo cha Afya Sina Kata ya Mafisa.
Miongoni mwaVifaaTiba vilivyotolewa katika Zahanati hizo, ni Darubini 5 (Microscope), Kifaa cha kutenganisha selamu na seli za damu( CentrifugeMashine 5), Kifaa cha kupimia sukari ( Glucopus ) 5, Kitanda cha kumuangalia mgonjwa (Examination bed 2)’.
Mhe. Abood, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. SamiaSuluhu Hassan kwa kuhakikisha wanawake wa Jimbo la Morogoro Mjini, wanajifungua kwenye mazingira salama.
Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga,amemshukuru Mbunge Abood, kwa Mchango wake hususani kwenye sekta ya afya huku akieleza kuwa Vifaa vyote tiba ambavyo wamevipokea vitakwenda kufanya kazi kama ilivyokusudiwa pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kukidhi mahitaji ya wananchi.
Naye Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Morogoro Mjini, Elizabeth Badi, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro amesema kuwa Manispaa itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali pamoja na Ofisi ya Mbunge katika kuboresha maisha ya wananchi kwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu afya kwa kutumia vikundi mbalimbali vya sauti za umma, kuwapa semina wataalamu wa afya na kutoa vifaa kwaajili ya Zahanati zote na kuboresha huduma za elimu shuleni.
Katika hatua nyingine licha ya kugawa vifaa tiba lakini amegawa jumla ya madawati 310 Shule ya Sekondari Mazimbu Mei 10-2024.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa