MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amefurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Wataalamu wa Manispaa ya Morogoro katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Kauli hiyo, ameitoa katika kikao cha Kawaida cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa Februari 08/2023.
Akizungumza katika Baraza hilo, Mhe. Kihanga, amesema miradi inayotekelezwa na Manispaa kupitia wataalamu ni mizuri na imeonesha na kuzingatia thamani ya fedha.
“Wataalumu wetu wanafanya kazi kubwa, tuwapongeze, miradi inakwenda vizuri, tumeona madarasa ya Pochi la Mama yamekamilika kwa wakati na watoto wetu wanasoma vizuri, endeleeni kuchapa kazi, tuna ndoto ya kuwa Jiji, bila kuwa na miradi ya uhakikka ndoto yetu itachelewa kutimia” Amesema Kihanga.
Katika hatua nyengine, amewataka Madiwani katika kuelekea Bajaeti ya fedha ya mwaka 2023/2024, wajipange vizuri na kutafakari kubuni miradi mikubwa ambayo itaongeza mapato ya Halmashauri.
“ Mwaka 2015/2020 Baraza la Madiwani lilifanya kazi kubwa ya kuibua vyanzo vikubwa vya mapato hadi tunafikisha makusanyo ya Bilioni 12 sio kazi ndogo, ni kazi yetu sisi tuliopo tuhakikishe tunabuni vyanzo vipya na vikubwa vitakavyo tuhakikishia makusanyo makubwa ya mapato , muda mnao Madiwani mjipange kuja na mikakati mikubwa tunapoelekea Bajeti ya fedha ya mwaka 2023/2024” Ameongeza Mhe. Kihanga.
Mwisho,amewashukuru Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwa kuendelea na moyo wa ujenzi wa Taifa kwa kuchangia michango mbalimbali ya Maendeleo, hususani katika Ujenzi wa Maboma ya Shule .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa