MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Watumishi Wanaotarajia kustaafu na waliostaafu mwaka huu kuwa karibu na taasisi za kidini katika mahubiri pamoja na kushauri Serikali na Vijana katika kutekeleza Miradi ya Uchumi kwa Manufaa ya Jamii na Taifa zima.
Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 25/2022 katika Baraza la uwasilishwaji wa taarifa za Kata Ukumbi wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Mhe. Kihanga, amechukua nafasi ya kuwapongeza Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kwa Ushirikiano Mkubwa Uliooneshwa Kwa Watumishi hao na kuwaomba wastaafu nao kuwa kioo kwa Jamii kama walivyoonesha maadili wakiwa kwenye ajira Serikalini.
Aidha, Kihanga, amesema upendo na amani vinatakiwa kuwepo ambapo Manispaa nayo inatakiwa kuendelea kuwatumia wastaafu kuendeleza miradi na Ushauri pasipo kuwatenga huku wastaafu hao wakitakiwa kuwa Makini na watu matapeli ambao wanaweza kuwashawishi wakatoa fedha za mafao ya uzeeni kwa watu ambao siyo sahihi na kupata hasara ambapo matokeo yake ni kufa kwa presha.
Hata hivyo, amewataka wastaafu kuepukana na marafiki wasiyo waaminifu wakiwemo watoto wao kwani matapeli wanaweza kutumia watoto wao kufanya utapeli wa mali za aina mbalimbali.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa