MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kupanda miti hususani katika maeneo yenye vyanzo vya maji ili kuondokana na tatizo la upungufu wa maji katika kipindi cha kiangazi.
Kauli hiyo,ameitoa Mei 21/2022 katika Kongamano la Wadau wa Mazingira Mkoa wa Morogoro lililofanyika katika Ukumbi wa Magadu Mess Manispaa ya Morogoro.
“Niwaombe sana wananchi wote wa Manispaa ya Morogoro, tuendelee kupanda miti, tumeona Serikali imetaka kila Wilaya kupanda Miti Milioni 1 la laki 5 sasa tuelekeze nguvu hiyo kupanda miti na kuitunza, tukifanya hivi tutarudisha Uoto wa asili katika vyanzo vya maji ambavyo vimeanza kupotea kutokana na baadhi ya Wananchi kuendesha shughuli zao pembezoni mwa vyanzo vya maji ikiwamo Kilimo” Amesema Mhe. Kihanga.
Mhe. Kihanga, amewataka Watendaji wa Kata na Mitaa kwa kushirikiana na Viongozi wa Mitaa kushirikiana kikamilifu kuhakikisha kwamba wanakemea vikali wanaoharibu mazingira kwa kukata miti hovyo na kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa vyanzo vya maji.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa