MKUU wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe Manispaa ya Morogoro, Dkt. Maneno Matawa, amesema mabaraza ya wazee yabebe jukumu la kujadili changamoto zao ikiwemo kujua ni wazee wangapi ambao wanatakiwa kupewa Vitambulisho vya Msamaha wa matibabu bure pamoja na utambuzi wa wazee wanaostahili kuingizwa katika mpango wa wanufaika wa TASAF.
Daktari Matawa amesema hayo tarehe 18.10. 2023 katika kikao kazi kilichofanyika kwenye Ofisi ya Kata ya Mzinga, mara baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa Majengo ya Huduma ya Kulaza Wagonjwa, Zahanati ya Konga Kata ya Mzinga ambapo pia amesema kwamba Manispaa inaendelea na jitihada mbalimbali za kuendelea kuboresha huduma kwa wazee hasa kwa kuwapatia vitambulisho vya matibabu bure (ICHF).
"Hii ni faraja kwetu kuona huduma zetu zinaendelea kuimarika. Ni mara yangu ya kwanza kuja kukagua ujenzi huu tangia niwasili Manispaa hivi karibuni lakini nimeona kazi kubwa inaendelea kufanyika chini ya usimamizi wenu, sisi kama Manispaa tutahakikisha kuwa ujenzi wa Majengo haya unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupatiwa huduma bora za afya" alieleza daktari Matawa.
Aidha, daktari Matawa amezipongeza Kata za Manispaa kwa kufanya maadhimisho ya mabaraza ya wazee na amewataka Watendaji wa Kata kuendelea kufanya utambuzi wa wazee kupitia mabaraza yao ya Kata ili wapatiwe vitambulisho vya msamaha wa matibabu vitakavyo wawezesha kupata huduma bila changamto yo yote katika vituo vya kutolea huduma za afya.
MWISHO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa