Mbunge wa Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaziz Abood, amesema kuwa Jimbo la Morogoro Mjini, limepokea Jumla ya kilomita 21.5 za Barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami kupitia Mradi wa TACTIC ambao ni Mradi wa Uboreshaji Miji.
Mhe. Abood, amesema kuwa , mradi huu umekwisha sainiwa na Serikali kuu ya Tanzania kupitia O-R TAMISEMI na Benki ya Dunia(WORLD BANK) ambapo Mradi huu utagharimu Fedha za kitanzania karibuni Bilioni hamsini(Bil.50) hii ikienda sambamba na ujenzi wa stendi ya magari eneo la station ya Reli ya mwendokasi (SGR) Kihonda kwa mwaka wa Fedha 2022/2023.
Miongoni mwa mgawanyo huo wa kilomita ni pamoja na K.m 17 Kata ya Tungi, K.m 3.5 Kilimanjaro -Kihonda kutoka Reli ya Mwendokasi (SGR), na K.m 1 ni kwenda Stesheni ya Reli ya Mwendokasi (SGR).
Aidha, Mhe. Abood, amesema Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imepewa Jukumu la kutafuta Consultant(Mshauri Mtaalam wa Kiinjinia atakayehusika na Upembuzi yakinifu wa Mradi) Kutangaza tenda na Kumpata Mkandarasi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa