MKURUGENZI Manispaa ya Morogoro, Sheilla lukuba,amepiga marufuku biashara kupangwa chini hususani bidhaa za vyakula.
Agizo hilo amelitoa Aprili 11,2020 kufuatia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Mhe. Regina Chonjo la kutaka bidhaa zinazouzwa masokoni zisimwagwe chini.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema kumekuwa na wimbi la Wafanyabiashara ambao sio Wastarabu wanaosambaza bidhaa za vyakula chini jambo ambalo sio zuri kwa afya ya mlaji na wanunuzi.
Amesema kuanzia Leo, bidhaa zote pamoja na za vyakula viwekwe juu ya meza. .
"Kuanzia leo ni marufuku bidhaa za vyakula kumwagwa chini,tunataka bidhaa zote katika masoko ziwekwe mezani, kuwekwa chini kuna uchafu wa maji machafu yanayotiririka ambayo yakigusa vyakula vijidudu vyote vinaingia humo na kumsababishia mlaji kupata magonjwa ya kuhara, ukizingatia kipindi hiki cha janga la Ugonjwa wa CORONA lakini yale magari yanayoingia Sokoni yanoyoleta viazi yaishie Nanenane na wauze kwa jumla , ili mkileta huku muwe na utaratibu maalumu, naondoka nikirudi nikakuta bado bidhaa za vyakula vipo chini naita Greda tunakwenda kuvimwaga dampo" Amesema Sheilla.
Katika hatua nyingine, ameitaka minada yote iliyopo Manispaa Morogoro kuweka ndoo pamoja na sabuni kwa ajili ya kunawia mikono na wakishindwa minada yote yani Kikundi pamoja na Sabasaba itawekwa siku moja.
"Mkuu Wa Wilaya, alishatoa maelekezo , sasa mimi kazi yangu ni kusimamia kama maagizo yametekelezwa, kikubwa zaidi katika Minada yote hakikisheni ndoo za kunawia Maji zinakuwa za kutosha na kuziweka kila kona ya kuingilia katika minada, pili ni lazima katika biashara zenu muachiane nafasi msirundikane lengo letu ni kuwakinga nyinyi pamoja na wateja wenu katika janga hili la Ugonjwa wa CORONA. " Ameongeza Sheilla.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa