Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba aongoza zoezi la uandikishaji wananchi katika daftari la wapiga kura kwa kujiandikisha katika mtaa anaoishi wa Nguzo ikiwa ni ishara ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo.
Mkurugenzi Lukuba ameeleza kuwa yeye ameamua kujiandisha katika mtaa wake ili kuhamasisha jamii kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji lililopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia tarehe 8-14/10/2019.
Aidha Mkurugenzi Lukuba ameeleza ni vyema wananchi wakajitokeza kwa wingi katika zoezi hili la uandikishaji ili waweze kuja kuchagua viongozi ambao watawasemea na kuwasaidia katika maendeleo ya mitaa yao husika.
Nawasihi pia watumishi wa taasisi mbalimbali kujitokeza kwa wingi hasa siku za mwishoni mwa wiki ambazo ni za mapumziko kujitokeza katika mitaa yao husika kujiandikisha ili kuweza kushiriki katika kuwachagua viongozi waliobora,"Alisema Lukuba"
Pia ametoa wito kwa wananchi kuwa itapofika kipindi cha kampeni ,kujitokeza kusikiliza kwa umakini na kuamua kuchagua viongozi ambao wataleta maendeleo katika mitaa yao.
Naye msimamizi wa uchaguzi Manispaa ya Morogoro Waziri Kombo ameeleza kuwa muitikio wa wananchi umekuwa mzuri toka zoezi lilipoanza na kuendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi.
Kombo ameeleza kuwa Manispaa ya Morogoro itafanya uchaguzi katika mitaa 294,na inatarajia kuandikisha wapiga kura 177,000,na alibainisha sifa za mwananchi kuandikishwa ni ni kuwa raia wa Tanzania,mwenye umri wa miaka 18 au zaidi,awe hana ugonjwa wa akili na atatakiwa kujiandikisha katika mtaa husika anaoishi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa