• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MKURUGENZI MANISPAA MOROGORO AAHIDI USHIRIKIANO NA WAMACHINGA ,BAADA YA KUKABIDHIWA CHETI NA SHIRIKA LA WAMACHINGA TANZANIA.

Posted on: November 5th, 2019

MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheila Edward Lukuba, ameahidi kuendeleza Ushirikiano dhidi ya Wafanya biashara ndogo ndogo maarufu Wamachinga kufuatia Shirika la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) kwa upande wa Manispaa ya Morogoro , kuikabidihi  Manispaa hiyo Cheti kutokana na ukaribu na ushirikiano mkubwa wa kuwawezesha Wamachinga kujiendeleza.

Akizungumza leo Novemba 5, 2019, Ofisini kwake, katika kumwakilisha upokeaji wa cheti hicho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa John K.Mgalula,  Mkurugenzi Sheila, amesema anatambua umuhimu wa Wamachinga , hivyo Manispaa yake itaendelea kushiriki na kuwa karibu na Wafanya biashara hao.

Amesema ni vyema Wamachinga wakathaminiwa, kwani hata Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amekuwa  mstari wa mbele katika mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara na kuwatambua kama kundi muhimu kuelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa kati.

"Nashukuru sana kwa mchango wenu, kwanza mmetupa heshima  Manispaa, mnatambua umuhimu wa Serikali yenu nasi tutazidisha mahusiano bora na rafiki kwenu ili kuhakikisha wafanya biashara wote mnanufaika  na mnakuwa na kipato katika biashara zenu, haiwezekani wachache wanufaike wengine muumie, tutawasimamia kama Mh Rais wetu Dkt John Magufuli anavyo wathamini, nakipokea cheti hiki kumwakilisha Mkurugenzi aliyepita ,  natumani taarifa zenu anazo, tusichoke kwenye changamoto tuambiane sisi kazi yetu ni kuwakwamua pale mnapo kwama" Amesema Sheila.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Sheila, amesema kundi hilo linatambulika kwa kupatiwa Vitambulisho vya Wajasiriamali kwa malipo ya Shilingi Elfu 20,000/=tu  kwa mwaka, hivyo wawe makini na wafanya biashara wanaojifanya wao ni Wamachinga kwa lengo la kukwepa kodi ya Serikali.

"Sisi Manispaa  tunahitaji kodi, kuna watu wajanja wajanja sana wanajifanya wamachinga  kumbe wanakwepa kodi, tukiwashtukia tutawashughurikia, tunahitaji kodi kwa ajili ya maendeleo, tuna miradi ya Hospitali, Shule, Maji, Maabara na mengineyo yote inahitaji fedha" Amesisitiza Sheila.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Shirika la Umoja Wamachinga Tanzania ( SHIUMA) , Ndugu Faustine France, amesema Cheti hicho ni kwa heshima ya Manispaaa pamoja na Mkurugenzi aliyepita kwa kuwatambua na kuwathamini.

"Naipongeza  Manispaa kwa kazi nzuri za ujenzi wa Taifa pamoja na usimamizi mzuri wa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ya Kimkakati , Jumuiya yetu tunaahidi kwa dhati kukupatia ushirikano  kama ilivyo kwa Mkurugenzi  aliyepita katika Manispaa yako, tupo tayari kufuata maelekezo yako na tutayafanyia kazi" Amesema Faustine.

 

Aidha, amesema licha ya kutoa cheti hicho, pia ugeni wao ulikuwa ni pamoja na kumkaribisha Mkurugenzi mpya kwa kumpa ushirikiano na kutambua wamachinga pamoja na Jumuiya yao kwa Maendeleo ya Manispaa ya Morogoro.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa