MKURUGENZI ManispaaMorogoro Sheilla Lukuba, ametoa msaada wa Chakula kwenye Makao ya kuleleaWatoto Yatima Mgolole katika kuelekea Sikukuu ya Christmas.
Vyakula hivyovimekabidhiwa na Afisa Ustawi Manispaa Morogoro, Rehema Malimi, Desemba22 /2020 katika Makao ya kulelea Watoto Yatima Mgolole .
Akizungumza kwa niabaya Mkurugenzi Manispaa Morogoro , Rehema Malimi, amesema msaada huo ameutoabinafsi ili kujumuika kwa pamoja na Watoto hao katika kusherehekea Sikukuu yaChristmas.
"Nimekabidhimsaada huu ambao amenituma Mkurugenzi Manispaa Morogoro ,Sheilla Lukuba,kuwaletea Watoto, amesema anatambua furaha ya Watoto hivyo katika kuonyeshayupo pamoja nanyi ameona alete hiki chakula ili tunaposheherekea sikukuu yaChristmas tujisikie tupo huru na watu Wenye furaha Kama zilivyo familianyengine, "Amesema Malimi.
Malimi, amesema kuwaManispaa Morogoro kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogorohaitawaacha nyuma Watoto hao kwani imekuwa ikifanya hivyo Mara kwa mara na kuwakaribu na Makao ya Watoto pamoja na Wazee wasio jiweza ili kuonyesha kuwaSerikali yao inawajali na kuwathamini.
Miongoni mwa vyakulavilivyotolewa ni pamoja na Mayai trei 5, Samaki Kilo 10, Sukari Kilo 25, Ungawa ngano Kilo 25, Mafuta ya kula Lita 10 pamoja na Maziwa ya Lactojeni Makopo3.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa