MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ameagiza Watumishi wote wa Halmshauri ya Manispaa ya Morogoro pamoja na Wakuu wa Idara kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais.
Hayo ameyazungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Wafanyakazi Manispaa ya Morogoro.
Amesema zoezi hilo wasiwaachie Wananchi pekee kwani wao wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi ili wajiandikishe na kutimiza haki zao za Kikatiba.
"Pamoja na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kujiandikisha, nanyie hakikisheni watumishi wote mnajiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura kwani zoezi hili ni muhimu kwa kila mmoja wetu" Amesema Sheilla.
Aidha, pia amewataka Wananchi kujitikeza kwa wingi Kwenda kituoni kuandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura.
Amesema miongoni mwa faidia za kujiandikisha katika uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ni pamoja na Kupunguza malalamiko ya wadau juu ya Daftari la kudumu la wapiga kura, Kuwafanya wapiga kura wajiamini kutokana na taarifa zao kuwa sahihi na salama, Kunapunguza malalamiko ya uchaguzi, Kupunguza vurugu wakati wa uchaguzi, Unajenga usawa na uwazi katika mchakato wa Uchaguzi, pamoja na Kunalifanya zoezi la uchaguzi likubalike
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa