MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amewahakikishia wananchi wa Manispaa ya Morogoro kua hakutakua na kero babaifu za huduma za jamii kutokana na kuwepo kwa mikakati madhubuti iliyowekwa na halmashauri hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
Ameyasema hayo Kupitia kikao cha Kawaida cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa Februari 08/2023.
Kupitia maswali yaliyoulizwa ya papo kwa papo na Madiwani wakipambania utatuzi wa changamoto zinazozikabili kata zao,Machela, amewatoa hofu Madiwani kwa kusema kuwa Manispaa ina mipango mizuri na utekelezaji utaanza mara moja kwakua fedha za Halmashauri zipo za kutosha.
Katika upande wa elimu , Machela, amewataka wananchi kuendelea kujitolea na kufanikisha upatikanaji wa maboma kwa ajili ya Madarasa na Serikali itamalizia kwa sehemu iliyobaki kwa asilimia miamoja ikiwa ni pamoja uezekaji na upatikanaji wa madawati.
Pia amewahakikishia kuwa swala la upungufu Madawati linakwenda kuisha hivi karibuni kwakuwa ni kipaumbele cha kwanza katika bajeti ya robo ya tatu inayoanza hivi karibuni, jumla ya shilingi 500 zimetengwa kwa ajili ya Madawati.
Kuhusu huduma ya afya, Machela, amesema mpango uliokuwepo ni kuhakikisha wanajenga majengo mawili makubwa ya Upasuaji katika Kituo cha afya Mafiga na Sabasaba.
“Tutaendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi wetu, mkakati wetu ni ujenzi wa majengo ya upasuaji, lakini suala la changamoto ya vifaa tiba katika Zahanati zetu, hilo tumeliona na Manispaa imetenga fedha kidogo kwa ajili ya ununuzi wa vifaa ambapo hivi karibuni tutaanza kusambaza huku tukisubiria vifaa vingine toka serikali kuu ambayo ndio ina dhamana ya kusambaza vifaa tiba baada ya Halmashauri kukamilisha ujenzi wa Zahanati ” Amesema Machela.
Akijibu hoja ya sintofahamu waliyonayo wananchi wa Kiegea kuhusu hatma ya umilki wa ardhi, amesema Baraza la Madiwani limepitisha ya kwamba kwa wananchi walioongezewa maeneo wasitozwe pesa yoyote kwa ongezeko hilo bali wamiliki bure kutokana na uhitaji wa wananchi wasio na uwezo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa