Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheilla Lukuba , amekabidhi TV Flat Screen pamoja na Kingámuzi cha AZAM kwa Kitengo cha Ustawi wa Jamii Manispaa ya Morogoro.
Tukio hilo la makabidhianao hayo limefanywa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Dr. Ikaji Rashidi, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro leo Aprili 9/2021 kwenye Jengo Jipya la Ofisi ya Ustawi linalotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi laki 750,000/= amevitoa ikiwa ni jitihada zake za kufanya maboresho katika Kitengo cha Ustawi ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kutoa huduma bora.
Ikaji, amesema lengo la kutoa Tv hiyo ni kuwafanya wateja wanaofika Ofisini kufuata huduma waweze kutazama vipindi mbalimbali vyenye kutoa elimu pamoja na kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea na kuona maendeleo yanayofanywa na Serikali.
Amesema kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, licha ya msaada huo lakini amekuwa mstari wa mbele sana katika kusaidia Idara ya Afya na Kitengo cha Ustawi kwani mara kwa mara amekuwa akijitoa kwa hali na mali kusaidia makao ya kulelea Watoto yatima pamoja na makao ya wazee kwa kuwapatia huduma mbalimbali ikiwamo huduma za vyakula pindi wanapohitaji huduma hizo amekuwa haachi nyuma.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Ustawi wa Manispaa ya Morogoro, Hamisa Kagambo, amemshukuru Mkurugenzi kwa msaada alioutoa kwani itawasaidia wateja wanaofuata hudma kuweza kupunguza msongo wa mawazo kipindi anapotoka nyumbani akiwa amekorofishwa au kuwa na jambo ambalo limekuwa na presha ya hali ya juu.
Kagambo, amemuomba Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro aendelee na moyo wa kuwasaidia kwani mbali na alichokitoa bado Kitengo hicho cha Ustawi kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za huduma huku akimtakia kazi njema katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Naye Mmiliki wa kituo cha kulelea watoto wadogo (day care) Rainball kilichopo Kata ya Kihonda Maghorofani, Abdallah Sakibu, amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, kwa kuwa mstari wambele kusaidia Ustawi wa Jamii kwa kutoa vifaa hivyo lakini kubwa zaidi kwa kuwajengea Ustawi wa Jamii jengo la Ofisi kwani sasa wanaamini Jengo hilo litakuwa suluhisho la kuweka usiri mkubwa baina ya wateja na wafanyakazi.
Amesema kuwa, awali wateja wamekuwa wakipata shida sana wanapofika Ofisi za Ustawi kwani wamekuwa wakipishana na watumishi wengi jambo ambalo linamfanya mteja kushindwa kuelezea tatizo lake kwa uwazi zaidi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa