Kama ilivyo ada kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi ufanyika usafi katika maeneo mbalilmbali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe Rais John Magufuli,leo tarehe 25/08/2018 mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Steven Kebwe ameungana na wafanyabiashara wa soko la Mawezi ndani ya Manispaa ya Morogoro kufanya usafi katika soko hilo.
Akiwa katika zoezi la usafi amewahimiza wananchi wote kukumbuka kufanya na kudumisha usafi wa maeneo ya kufanyia biashara ili kumfanya mnunuzi kuwa na mori wa kununua bidhaa katika soko hilo.
“Lengo kuu ni kuepusha wananchi kupata magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kujitengenezea utamaduni wa uwajibikaji binafsi wa kutunza mazingira yetu,” alisema Dkt Kebwe.
Aidha Dkt Kebwe amewaagiza wafanya biashara kuendelea kulipa ushuru wa vikazi ili Halmashauri iweze kupata mapato na kuweza kuwaboreshea maeneo ya kufanyia biashara ikiwa pamoja na choo kilichopo katika soko hilo.
"Naagiza kila mfanyabiashara kulipa ushuru ikiwa ni utekelezaji wa jukumu lake"alisema Dkt Kebwe.
Sambamba na hayo Dkt kebwe alisikitishwa na taarifa za kuporomoka kwa mapato yanayopatikana katika soko hilo na kueleza kuwa amekuwa mfuasi mzuri wa kufuatilia mapato katika soko hilo ila anashangazwa na baadhi ya wafanya biashara wanaogomea kulipa ushuru wa vikazi.
Dkt kebwe amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa Ndg John Mgalula kufuatilia kwa umakini kuhusiana na mapato ya soko na ametaka mapato yapande na siyo kushuka,kwakuwa mapato hayo ndiyo utumika kufanya maendeleo katika soko hilo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa