Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr.Kebwe Stephen amemtaka Mkurungezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro John Mgalula, kuweka mkakati wa haraka na kuanza mara moja kujenga shule mpya tano za msingi, ili kupunguza msongamanouliopo, ambapo baadhi ya shule zina wanafunzi zaidi ya 2000 na bado kunauhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa.
Dr Kebwe ametoa agizo hilo katika mkutano wake na walimu wakuu washule za Msingi na sekondari,maafisa elimu Kata,na wadau wa elimu manispaa yaMorogoro, ambapo amesema kulingana na ongezeko hilo la wanafunzi, hakuna sababuya kuongeza vyumba vya madarasa, bali ni kujenga shule nyingine tano, ambazozitasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi.
Mkuu huyo wa Mkoa, amesema kwa sasa Manispaa ya Morogoro ina jumlaya wanafunzi 56,755 ambao wanahitaji vyumba vya madarasa 1,252 lakini vilivyoponi 620 hivyo kupelekea kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 632.
Kwa upande wake Afisa elimu msingi Manispaa ya Morogoro Bw. AbdulBuhety amesema endapo maagizo ya Mkuu wa Mkoa yatafanyiwa kazi, basi kunauwezekano mkubwa wa kupunguza msongamano wa wanafunzi mashuleni kutokana nauchache wa vyumba vya madarasa, kwani kuna baadhi ya shule zina zaidi yawanafunzi 2000, hivyo endapo kutaongezwa kwa shule hizo tano, kutasaidiakuondokana na tatizo hilo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Dr Kebwe Stephen, amewatakawakuu wa Shule Msingi na Sekondari pamoja na viongozi wengine wa Elimu Mkoanihapa,kuhakikisha wanazingatia waraka namba sita wa Mwaka 2016, unaotoa Mwongozowa elimu bure, ili kuepukana na uendeshaji wa michango mashuleni ulio kinyumena waraka huo.
Aidha mkuu wa mkoa amewatahadharisha viongozi wenye dhamanaya elimu kuzingatia waraka namba sita wa mwaka 2016 unao toa mwongozo wa elimubure ili kuepuka uendeshaji wa michango mashuleni ulio kinyume na waraka huo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa