SHIRIKA la kuhudumia wazee Mkoani Morogoro (MOREPEO) limeuomba uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuharakisha mchakato wakuwatambua wazee wote waliopo ili kuweza kuunda mabaraza maalumu ya wazee.
Hayoyalisemwa jana na Mkurugenzi wa Shirika hilo Samson Msemembo wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wazee ambayoufanyika kila mwaka.
Alisemakuwa manispaa inapaswa kuwatambua wazee wote waliopo ili kuundwa mabaraza hayo jambo ambalo litawasaidia wazee kukutana na kujadili masula na changamoto mbalimbali za wazee na kisha kero zaokuzifikisha katika ngazi ya maamuzi.
‘’Tumeshatoa miezi miwili kwa Halmashuri ya Manispaa ya Morogoro kusimamiana kuhakikisha mabaraza hayo yanaundwa ‘’alisema Msemembo .
Hata hivyo alisema kuwa wazee mkoani Morogoro wanakabiliwa na changamoto kubwa yakulea watoto yatima na wale wenye maambuki ya virusi vya ukimwi huku wakikosa rasilimali fedha ya kuendesha maisha yao ya kila siku .
Kwaupande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga aliwataka wazee kuwa wavumilivu wakati wakisubiri mchakato wa mabaraza hayo kuundwa kila kata .
‘’Nawaomba wazee kuwa wavumilivu wakati wakisubiri mabaraza haya kuundwa kwani yatawapa fursa wazee kukutana na kuwa na Mwenyekiti wao‘’alisema Kihanga.
Hatahivyo Mstahiki Meya aliwashukuru wadau mbalimbali na mashirika yanayosaidiawazee kwani serikali peke yake haiwezi kwaniwazee wanapaswa kusaidiwa kwani walishalitumikia taifa kwa muda mrefu .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa