Msimamizi wa uchaguzi Manispaa ya Morogoro,ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Emmanuel Mkongo, ametoa maelekezo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, Mwaka 2024.
Maelekezo hayo ya uchaguzi ameyatoa Septemba 26-2024 kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi Kuu ya Manispaa ya Morogoro katika Mkutano wa wadau wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa Vyama vya Siasa.
Mkongo, ameeleza,Uchaguzi wa Serikali za mitaa utafanyika tarehe 27 Novemba 2024 na Uandikishaji utaanza tarehe 11 hadi 20 Octoba 2024 katika Mitaa 294 na Kata 29 ndani ya Manispaa ya Morogoro ambapo Vituo vya kuandikisha wapiga kura vitafunguliwa kuazia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Aidha,Mkongo, amewasisitiza wakazi wote wa Manispaa ya Morogoro , wenye sifa ya kupiga kura kujiandikisha ili kushiriki uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa Novemba 27-2024.
Pia ametoa wito kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro wenye Umri wa Miaka 21 au zaidi wanaotaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa Mitaa na ujumbe kuchukua fomu za kugombea zitakazo patikana kwenye ofisi ya msimamizi msaidizi wa uchaguzi kwenye Mitaa yao.
Hata hivyo,amesema kuwa fomu za maombi ya kugombea Uenyekiti wa Mitaa na wajumbe zitachukuliwa tarehe 1 hadi 7 Novemba 2024 saa 1:30 asubuhi ambapo mwisho wa kupokea fomu ni saa 10:00 kamili jioni huku Fomu hizo zikitolewa kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
"Uchaguzi wetu utakuwa huru na haki, kanuni zote za uchaguzi zitafuatwa, na majina ya wagombe yatabandikwe kwenye ubao wa matangazo katika Ofisi zao za Mitaa, nitoe rai kwa wananchi wote wenye sifa za kugombea wachukue fomu ili mradi uwe mtanzania,miaka 21 na kuendelea,uwe na akili timamu,ujue kusoma vizuri na kuandika lugha ya kiswali au kingereza na uwe mwanachama wa chama chochote cha siasa" Amesema Mkongo.
Mikutano ya Kampeni itafanyika kwa siku 7 kuanzia tarehe 20 hadi 26 Novemba 2024 ambapo itaanza saa 2:00 asubuhi na kumalizika saa 12:00 jioni ya kila siku ya Kampeni.
Mkongo,amehitimisha kwa kutoa wito Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa amani kulingani na kanuni ya 35(6)mtu yeyote hataruhusiwa kubaki eneo la kupiga kura baada ya kupiga kura.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa