• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO-DC MSULWA

Posted on: October 14th, 2020

MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amewataka Wananchi pamoja na Viongozi mbalimbali kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo.

Kauli hiyo ameitoa leo Oktoba 14, 2020 , wakati wa Tamasha la kumuenzi Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye Viwanja vya Mnada wa Nyama Choma Nanenane Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na Waandishi wa habari,amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wananchi, viongozi pamoja na wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa kuwa wazalendo kwa nchi, uvumilivu, kudumisha upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.

“Kupitia kumbukumbu hizi sisi watumishi wa Umma, Wananchi , Viongozi mbalimbali pamoja na Wanasiasa , tunatakiwa kujifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika, wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine, leo ni miaka 21 tangia atutoke Kipenzi chetu lazima tujitafakari dhdi ya kauli zake alizotuachia Baba wa Taifa, ” Amesema DC Msulwa .

DC Msulwa, ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa manufaa ya taifa.

“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa nyumba na Jeshi kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi, sasa haya ambayo tumeyaona yanatufundisha nini tukifanye kwa Taiafa letu ili liweze kupiga hatua mbele ” Amesisitiza DC Msulwa.

Aidha, DC Msulwa, amebainisha kuwa Wilaya yake kwa kushirikiana na Viongozi wa Halmashauri wataendelea kumuenzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa viongozi mbalimbali wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.

“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, Viongozi wanapaswa kuwaheshimu wananchi na kipindi hiki tunaelekea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 28,2020 , niwaase Wanasiasa wafanye Kampeni za kistaarabu na kuwaheshimu wale ambao wanawachagua kupitia chaguzi mbalimbali, matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao na sio kleta fujo ambazo zitakuwa na matokeo mabaya kwa Jamii na kutia doa Taiafa letu linaloongoza kwa amani Duniani kote ” Ameainisha DC Msulwa.

Kwa upande wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mstaafu, Mhe. Steven Mshishanga, amesema kuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mtu wa kipekee kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Mashishanga, amesema kuwa Mwalimu Nyerere alipigania uhuru wa nchi za Afrika na haki ya kijamii ambapo alikuwa kielelezo cha uongozi kwa nchi zote za Afrika katika mapambano yao ya uhuru na hamu ya amani, uhuru na maendeleo ya kiuchumi.

“Kama kiongozi mwenye busara, Mwalimu alichangia sana katika mjadala kuhusu pengo la maendeleo ya kiuchumi baina ya mataifa ya Kaskazini na yale ya Kusini mwa dunia, kwa hiyo niwapongeze sana Uongozi wa Wilaya na Manispaa kwa kunialika hapa na kufanya tukio kubwa kama hili, Hafla ya leo ni muhimu, kwani Mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi mwenye uadilifu, ujasiri na shujaa wa uhuru wa Afrika” Amesema Mashishanga.

Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amesema kuwa watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hivyo wana kila sababu yakujifunza zaidi.

Lukuba ,amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.

Sherehe hizo za kumbukizi za Mwalimu Nyerere, zilihududhuriwa na Viongozi mbalimbali ikiwemo Viongozi wa vyama vya Siasa ambapo katika Tamasha hilo liliambatana na Uzinduzi wa Mnada wa Nyama choma Nanenane Kata ya Tungi ambapo wasanii mbali mbali walitoa burudani ikiwamo Msanii wa Singeli Msaga Sumu pamoja na Wasanii wa ndani wa Manispaa ya Morogoro wakiongozwa na MC Hamza.

 Mnada wa Nyama Choma utakuwa ni endelevu ambapo utakuwa unafunguliwa kila Jumapili kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi 12:30 jioni

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa