Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2021umetembelea miradi 7 yenye thamani ya Tsh 1.355,918,110.96 katikaWilayayaMorogoro.
Katika miradi hiyo ambapo mradi wa 1 kati ya hiyo wenye thamani ya Tshs. 648,175,470.96 umefunguliwa, miradi 2 yenye thamani ya Tshs. 156,418,940.00 imewekewa mawe ya msingi ,miradi 3 yenye thamani ya Tshs. 81,123,700 imekaguliwa na kuonwa na mradi 1wenye thamani ya Tshs. 470,200,000.00 umezinduliwa ambapo kati ya fedha hizo , Serikali Kuu imechangia Tshs.1,080,093,900 Halmashauri Tshs. 207,987,990.96, Wahisani Tshs. 2,000,000.00 na wananchi Tshs. 26,829,340.00.
Miongoni mwa miradi hiyo iliyotembelewa na Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Wilaya ya Morogoro ni pamoja na Mradi wa Kitega Uchumi Mbadaraka Mwinshehe (DDC), Ujenzi wa Mtaro wa kumwaga Maji machafu Mjini Kati, UjenziwaVyumba 4 vya Darasa Shule Mpya ya Sekondari Mazimbu, Mradi wa ushonaji wa Viatu Tungi Youth Initiatives Nanenane, Mradi wa Maji RUWASA Mikese, Kituo Jumuishi cha huduma za pamoja (One Stop Centre Mafiga ), na Kiwanda cha Usindikaji Maziwa Mtego wa Simba.
Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 ,umeongozwa na Kiongozi wa Mbio hizo Luteni Josephine Paul Mwambashi pamoja na wakimbiza mwenge wenzake.
Ikumbukwe kuwa Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 katika Wilaya ya Morogoro, ulitembelea jumla ya miradi 11 yenye thamani ya Tshs. 52,006,789,825 ambapo mradi 1 kati ya hiyo wenye thamani ya Tshs.154,350,680 ulifunguliwa, na miradi 4 yenye thamani ya Tshs.48,379,104,551.22 ilikaguliwa na kuonwa na miradi 4 yenye thamani ya Tshs. 3,067,670,594.00 ilizinduliwa na miradi 2 yenye thamani ya Tshs 405, 664,000 iliwekewa Mawe ya Msingi ambapo kati ya fedha hizo za miradi iliyotembelewa , Serikali Kuu ilichangia Tshs. 10,558,831,434.62, Halmashauri Tshs. 665,278,280, wananchi Tshs.15,184,000.00 na wahisani Tshs.40,767,496,111.00 miradi yote 11 iliyopitiwa na Mbio za Mwenge inaendelea vizuri katika kutoa huduma.
Ujumbe wa Mwenge wa uhuru wa mwaka 2021 ‘TEHAMA ni Msingi wa Taifa Endelevu, Itumie kwa usahihi na Uwajibikaji’.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa