Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Mhe.Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo March 1,2025 amezindua uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura katika kituo cha shule ya Msingi Mafiga B Manispaa ya Morogoro na kushuhudia wananchi wengi wakiwa wamejitokeza kuboresha taarifa zao.
Jaji Mwambengele amewataka wananchi ambao wanapaswa kuboresha taarifa zao kufika katika vituo vilivyopo katika maeneo yao kuboresha taarifa zao mapema na sio kusubiri hadi siku ya mwisho ya Machi 7.
Vituo vilivyotembelewa na Mwenyekiti huyo wa Tume Huru ya Uchaguzi ni Pamoja na kituo cha Mafiga B,kituo cha Ukwele kata ya Mafiga ,Kituo cha mtaa wa Ukwele kata ya Sultan Area,kituo cha Wamo kata ya Boma,Kituo cha Tushikamane kata ya Lukobe.
Zoezi hili la uboreshaji taarifa katika Daftari la kudumu la wapiga kura limeanza Machi 1 na litahitimishwa Machi7.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa