MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wamemthibitisha Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Mhe.Seif Zahoro Chomoka , aliyeshinda kwa kishindo kwa kupata kura zote baada ya Baraza hilo kumthibitisha.
Uthibitishaji huo wa Naibu Meya pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbalimbali umefanyika katika Ukumbi wa Manispaa Agosti 15-2024 katika Baraza la Madiwani la kukamilisha mwaka wa fedha 2023-2024.
Akizungumza mara baada ya uthibitisho wa kuwa Naibu Meya , Mhe. Seif Chomoka, amelipongeza na kulishukuru Baraza kwa kumthibitisha pamoja na kuwapongeza Wenyeviti wa Kamati zote waliopita kwa kishindo katika kinyanganyiro hicho ambapo Kamati ya Huduma za Uchumi,Elim una Afya alichaguliwa Mhe. Majuto Mbuguyu, na Kamati ya Mipango Miji na Mazingira alichaguliwa Mhe. Amini Tunda huku Kamati ya Maadili kwa Madiwani ikichukuliwa na Mhe. Thomas Butabile na Kamati ya Kudhibiti Ukimwi itaongozwa na Naibu Meya kwa mujibu wa muongozo.
Mhe. Chomoka, amelishukuru Baraza la Madiwani kwa kuonesha imani nae, ambapo amewaahidi madiwani wa Halmashauri hiyo kuwapa ushirikiano na kutetea maslahi ya Madiwani wote pamoja na wananchi kwa ujumla.
Aidha, Mhe. Chomoka,amesema atafanya nao kazi Madiwani wote kwa ushirikiano bila kuweka matabaka katika kufanya kazi za chama na Serikali na kuakikisha Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro inasonga mbele katika makusanyo ya Mapato na miradi ya Serikali na kutimiza adhima yake ya kuwa Jiji.
Pia, Mhe. Chomoka,amewapongeza viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Morogoro Mjini akiwemo Katibu na Mwenyekiti wake pamoja na mkuu wa Wilaya ya Morogoro ambapo amesema yeye ni Mtumishi wa Madiwani wote hivyo atawapa ushirikiano mkubwa.
Mwisho,Mhe. Chomoka,amewaomba madiwani waendelee kumuamini katika utekelezaji wa majukumu yake kwani moja ya jukumu kubwa ni kuhakikisha anamsaidia Meya majukumu yake kikamilifu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii, Mhe.Majuto Mbuguyu,ambaye ni Diwani wa Kata ya Uwanja wa Ndege, amewashukuru Madiwani kwa umoja wao na kuahidi kushirikiana nao bega kwa bega ili kuakikisha wanamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, Halmashauri hiyo iweze kusonga mbele katika kusimamia miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewapongeza Wenyeviti Kamati zote waliochaguliwa na kuwataka kufanya kazi pamoja kuakikisha Halmashauri hiyo inafikia malengo yake katika sekta zote .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa