WANANCHI wa Manispaa ya Morogoro wametakiwa kulipa ada za taka kwa madai kuwa kutofanya hivyo kunapelekea taka kujaa sana mitaani jambo ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya milipuko.
Hayo ameyazungumza mwenyekiti wa kamati ndogo ya mazingira Manispaa ya Morogoro,Mhe. Rashid Matesa, Oktoba 15-2024 katika ziara ya kamati hiyo ya kuangalia hali ya usafi mitaani kwa kampuni zilizopewa kandarasi za usafishaji wa Mji.
Matesa,amesema kuwa kwa sasa sheria ipo wazi ya kila kaya inalipa shilingi 3000/= hivyo ni wajibu wa wananchi kulipa ili kuweka mji safi.
"Sheria hii ni wajibu wa wananchi kuifuata,tunataka kuwa Jiji, hatuwezi kuwa Jiji kama bado Mji wetu nimchafu, tukilipa taka kwa wakati tunawatia nguvu wadhabuni wetu wa uzoaji wa taka ili wafanye kazi kwa ufanisi ,tusipolipa kwa wakati taka zitandelea kuzagaa mitaani na kusababisha magonjwa ya milipuko" Amesema Mhe. Matesa.
Kamati hiyo mara baada ya kumalizika kwa majumuisho,wamesema watahakikisha elimu ya ulipaji wa ada ya taka inazidi kutolewa kwa jamii ili kuwarahishia utendaji kazi wadhabuni wa uzoaji wa taka.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa