Ofisi ya Waziri Mkuu imesema , masuala ya udhibiti wa maabukuzi ya virusi vya ukimwi ni budi yaendelee kupewa kipaumbele kuanzia ngazi ya jamii , wilaya , mkoa , kitaifa ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia lengo la kimataifa la 90-90-90.
Hivyo, ni kwa maana ya ( asilimia 90 ya wanaoishi na VVU watambue hali zao , asilimia 90 ya WAVIU wawe wameanza dawa za kupunguza makali ya VVU na asilimia 90 ya walianza dawa wapunguze kiwango cha virusi mwilini) ifikapo 2020.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri mkuu , Paul Sangawe alisema hayo ( Okt 18, 2019) baada ya kuwasilishwa taarifa ya Uratibu wa Ukimwi ya Manispaa ya Morogoro .
Timu ya ujumbe wa maofisa kutoka Ofisi ya waziri mkuu, Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) pamoja na TAMISEMI pia walitembela Konga ya Manispaa ya Morogoro .
Sangawe alisema , ni muhimu kwa wakati huu kuunganisha wadau wa kuchangia shughuli za udhibiti wa Ukimwi ili kuweza kupewa kipaumbele kuanzia ngazi ya wilaya , mkoa na taifa .
Hata hivyo aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa kutenga bajeti na kuzitoa fedha hizo na kutumika , lakini ni vyema kujua jinsi zilivyotumika na kama zimeweza kuwasaidia walengwa .
“ Lazima kuwe na muunganiko wa kutengwa bajeti, utoaji wa fedha na matumizi yake iwapo yanawanufaisha walengwa “ alisema Sangawe.
Mbali na hayo alitaka mpango wa miaka mitano wa lishe unaotekelezwa katika Ofisi ya Waziri mkuu kuwa shughuli zake ziendelee kwa kushirikiana na wadau wengine licha ya mradi wa Sauti Yetu ufadhili wake kumalizika tangu Septemba mwaka huu (2019).
Naye Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathimini kutoka TACAIDS , Dk Jerome Kamwela akiwa katika Konga ya Manispaa ya Morogoro eneo la Kata ya Mbuyuni ,alisisitiza umuhimu wa wadau mbalimbali na jamii kuongeza nguvu juu ya kudhibiti ongezeko la maambukizi ya VVU.
Awali, Mwenyekiti wa Konga Manispaa ya Morogoro , Kellen Mpesa katika taarifa yake alisema , moja na jukumu lake ni kuhamasisha na kuunda vikundi vya WAVIU , kuhamasisha upimaji wa VVU kwa jamii , kuwaibua na kusaidia wagonjwa ambao wamepotea kwenye huduma bila taarifa zozote na wanaougua majumbani .
Pamoja na hayo alisema , Konga ya Manispaa imeunda vikunzi zaidi ya 20 na 11 na kati ya hivyo nane vinajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi vikiwa na wanachama 172 kati hao 145 wanawake na 27 wanaume.
Katika hatua nyingine , Asasi ya kiraia inayojishughulisha na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI pamoja na watu wanaoishi katika mazingira magumu HACOCA iliyopo Manispaa ya Morogoro imeweza kuwafikia watu 15,058 kati ya 16,716 waliolengwa kufikiwa katika kipindi cha mwaka 2016/2019
Mratibu wa Mradi wa kizazi kipya katika Asasi hiyo, Veronica Anonsisye alisema hayo kwa wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri mkuu , Tacaid na Tamisemi waliofanya ziara ya tathimini ya baadhi ya miradi ya UKIMWI mkoani Morogoro .
Kwa mujibu wa Mratibu wa Mradi wa Kizazi Kipya wa Asasi hiyo kuwa , watu hao wamejengewa uwezo katika masuala ya kiuchumi, lishe bora , elimu na dawa za kufubaza maambukizi ya virusi vya UKIMWI
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa