HIVI karibuni Manispaa imepokea tena kiasi cha Shilingi bilioni 1.620,000 kupitia pochi la mama kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Fedha hizo zimetolewa kwa mwezi Septemba kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 81 ya kidato cha kwanza watakaoingia mwakani 2023.
Katika fedha hizo ambazo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezitoa kwa ajili ya Ujenzi wa madarasa,, Manispaa ya Morogoro imeunga mkono juhudi za Mhe. Rais kupitia mapato yake ya ndani imeweza kuongeza madarasa 2 na kufanya jumla ya madarasa 83 ambayo asilimia kubwa ya madarasa pamoja na Meza na viti vimekamilika.
Kwa takwimu hizo, ujenzi wa vyumba vya madarasa 83 vimegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1 na milioni 660 na viko tayari kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.
Hii ni mara ya pili kupokea fedha ,ikumbukwe Manispaa ilipatiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 86 ya Uviko 19.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa