MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Fatma Mwasa, amewataka Wananchi wa Mkoa wa Morogoro kupanda miti kwa wingi itakayosaidia kutunza mazingira ili kwenda sambamba na mpango wa Serikali wa upandaji wa miti kuzuia athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Rai hiyo ameitoa Septemba 10/2022, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kimkoa ya usafi wa Mazingira pamoja na upandaji wa Miti ambapo Kampeni hiyo ya upandaji wa miti ataizindua hivi karibuni .
Akizungumza na Wananchi pamoja na Viongozi mbalimbali na watendaji waliojitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni hiyo ya usafi Kimkoa, Mhe. Mwasa, amewaasa watendaji wa serikali na wananchi kuhakikisha wanapanda miti, wanaitunza na kuilinda ili kuwa na mazingira yaliyo salama.
RC Mwasa, amewataka watendaji wa serikali kuhakikisha wanakamata wananchi wote wanaovunja sheria za mazingira na kusababisha uharibifu kwa kuchafua mazingira hovyo na kutupa taka katika maeneo yasiyoruhusiwa.
" Hili la Miti nitalisimamia kikamilifu, tumeanza na hili la usafi lakini hili la miti nitahakikisha tunatoa miti kwa kila mwananchi katika nyumba yake ili wapande tena hiyo miti ni ya matunda ili wananchi wanufaike vizuri, jukumu lenu ni kuhakikisha kwamba mnaitunza ili iweze kutusaidia baadae" Amesema RC Mwasa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa