Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa ameipongeza Taasisi ya Fountain Gates Schools kwa kuonesha nia ya kuwekeza katika michezo Mkoani Morogoro na kuahidi kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa nia hiyo inatimia.
Mhe. Mwassa ameyamesema hayo Aprili 12, 2023 wakati akiwapongeza wachezaji na viongozi wa timu ya wanawake ya Fountain Gates ambayo imechukua ubingwa wa kombe la Afrika kwa mashindano ya Shule za Sekondari mwaka 2023 baada ya kukutana na Mkuu huyo wa Mkoa Ofisini kwake.
Mhe. Fatma Mwassa amesema anaipongeza Taasisi ya Fountain Gates kwa wazo la kuweka kituo cha michezo Mkoani Morogoro kwani amebainisha kuwa kufanya hivyo kutaibua na kuendeleza vipaji vya watoto hususani wakike na kukuza soka la wanawake hapa nchini.
“...kubwa lililo tufurahisha zaidi ni nia ya Fountain Gate ya kuwekeza katika Sports Accademy hapa kwetu Morogoro, tunawakaribisha sana na tupo tayari kushirikiana nanyi....na tutahakikisha ndoto yenu inatimia...” Amesema RC Mwassa.
Sambamba na hilo Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya shule za Sekondari barani Afrika kwa upande wa wanawake huku wakitoa mchezaji bora wa mashindano hayo, mfungaji bora na kipa Bora hivyo amewapongeza viongozi wa timu hiyo kwa kujitoa kwao, kuiandaa timu hiyo hadi kutwaa ubingwa huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wakuu wa Shule za Fountain Gates Tanzania Bw. Joseph Mjingo amesema mafanikio wanayoyapata ni kutokana na sera nzuri ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan husuan katika utekelezaji mzuri wa Mtaala wa elimu na michezo kwa kuifanya michezo kuwa sehemu ya vipindi darasani.
Nae, Naodha wa timu hiyo Felista Richard amesema ushindi walioupata ni kutokana na ushirikiano kutoka Serikalini na kujituma kwao uwanjani huku akiiomba Serikali kutoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao ili waweze kuyafikia malengo waliojiwekea.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa