MKUU wa Mkoa waMorogoro, Mhe. Loata Sanare,amewataka Wazazi kufanyia kazi kwa vitendomaazimio mbalimbali yanayotolewa katika Vikao vya Kamati za Shule ilikuinua ubora wa Elimu.
Hayo ameyasema leoSeptemba 28,2020 wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya Ujenziwa Madarasa wa Shule ya Msingi Juhudi Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza naWaandishi wa habari, Sanare, amewataka Wazazi kuwa mstari wa mbele katikakutimiza maagizo na yatokanayo yote yaliyojadiliwa katika vikao vya Kamati zashule ili kuweza kuinua ubora wa elimu .
RC Sanare, amesemani muhimu kwa Wazazi wanaoshiriki katika Vikao vya kamati za shule kuyachukua maazimio yatokanayo na kikao katika kutekeleza kwa Vitendo yaleyaliyoazimiwa jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamotombalimbali zinazoikumba Sekta ya Elimu.
"Nimeona nifike hapa tujadili kwapamoja ili Kudumisha Ushirikiano baina ya Walimu na Wazazi katika kuhakikishakuwa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu ikiwemo utoaji wachakula inapatiwa ufumbuzi ikiwamo uzingatiaji utoaji wa Elimu ya awali,Uboreshajiwa miundombinu pamoja na kuzingatia utekelezaji wa maazimio yanayotokana naKamati za shule, niwaombe Wazazi hawa ni watoto wetu wanahitajielimu bora sasa kama sisi tutakwama hata elimu bora hawa watoto watakosaSerikali inafanya kazi kubwa ya kuimarisha elimu yetu kwa Watoto lakini kamawazazi pia tunayo majukumu ya kufanya kwa upande wetu ikiwamo kuchangia katikaujenzi na michango ya Chakula kwa Watoto wetu wawapo shuleni na ujenzi wamadarasa " Amesema RC Sanare .
Hata hivyo, katika kuhakikisha Ujenzi waMadarasa 3 yaliyobakia yanakamilika , amesema kupitia Ofisi yake kushirikianana Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi waManispaa ya Morogoro, kuchangia kiasi cha Shilingi milioni 20 ambapo milioni 17zilizobakia Wazazi watachangia kwakuwa hadi hatua iliyopo nguvu zote zimetokaSerikalini.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe.Bakari Msulwa, amewataka Wazazi wa Wanafunzi kujitoa kwa moyokuchangia Chakula Shuleni ili kuwawezesha watoto kupata chakula cha kutoshajambo litalaowawezesha watoto hao kuwa na Afya nzuri hali itakayowaezeshakufanya vizuri katika masomo yao na hivyo kuinua ubora wa Elimu .
DC Msulwa, amewataka Wananchi kutoaushirikiano wa kutosha kwa Walimu ikiwa ni sambamba na kujenga mazingira mazuriyatayowezesha Walimu na Watumishi katika Sekta ya Elimu kupenda mazingira yakazi jambo litakalosaidia kuinua ubora wa Elimu.
Shule ya Juhudi ni miongoni mwa shulepacha ya msingi Lukobe ambayo mpaaka sasa ina jumla ya madarasa 3yaliyomaliziwa na Wanafunzi wanasoma ambapo madarasa 3 yapo katika hatua yaupauaji .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa