MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela,ameipongeza Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiya Muslim Jama'at Tanzania iliyopo Morogoro kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kusaidia jamii.
Kauli hiyo ameitoa Julai 11/2022 , mara baada ya Jumuiya hiyo kufika Ofisini kwake na kumpatia zawadi ya Mkono wa Eid Al Adha.
Akizungumza juu ya Jumuiya hiyo, RC Shigela, amesema amefurahishwa na kazi wanazozifanya Ahmadiya ikiwamo kusaidia Serikali katika kuimarisha huduma za kijamii kama vile afya kwa kujenga shule na kujitolea kwa jamii zenye uhitaji.
"Nimeona niliseme hili wazi mambo mnayoyafanya ni ya uchamungu zaidi, hongereni sana kwa kazi, najua Serikali yetu ina vitu vingi inafanya hivyo haiwezi kumaliza vyote, vitu vyingine tunawategemea nyie wadau kuisadia Serikali yenu ili kuweza kufikia mafanikio, endeleeni na moyo huo huo ,Ofisi ya Mkoa tutaendelea kutoa ushirikiano dhidi yenu "Amesema RC Shigela.
Aidha, ameyaomba mashirika na Taasisi zingine yakiwemo madhehebu ya dini kuelekeza misaada mbalimbali kwa Wananchi wenye uhitaji maalumu ili kutengeneza furaha na kudumisha umoja baina yao na wenye uhitaji.
Naye , Mkuu wa Chuo cha Jumuiya ya Ahmadiya Morogoro, Sheikh Abid Mahmood Bhatti, amesema amepokea shukrani hizo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa msaada huo umetolewa kuunga mkono wito wa Serikali inayohimiza mashirika,taasisi,na watu binafsi kutoa misaada kwa jamii yenye uhitaji.
"Jumuiya ya Ahmadiya ni moja ya sehemu inayojihusisha na utoaji wa misaada mbalimbali ikiwemo ya kiafya,kielimu na kijamii kwa kuwafikia watu wenye uhitaji, hivyo leo tumeona tuzunguke kwa Taasisi zetu za Serikali kuwapatia Viongozi wetu mkono wa Eid al adha, ambapo kufanya hivi ni moja ya utekelezaji wa misingi ya dini , kwani sisi tumekuwa tukifanya hivi kila ifikapo siku ya Eid kama hii na tumekuwa tukijumuika na ndugu zetu kuhakikisha kwamba tunakuwa nao pamoja katika kusheherekea sikukuu hii " Amesema Bhatti.
“SENSA KWA MAENDELEO ,JIANDAE KUHESABIWA TAREHE 23/08/2022”
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa