MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amezindua mpango wa Chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya Miaka 5 Manispaa ya Morogoro.
Uzinduzi huo, umefanyika Mei 18/2022 katika Kituo cha Afya cha Sabasaba kilichopo Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, RC Shigela,amesema takribani zaidi ya watoto 400,000 wenye umri chini ya miaka mitano wanatarajiwa kufikiwa / kupatiwa chanjo ya kupooza (Polio) katika Mkoa wa Morogoro.
"Kumekuwa na upotoshaji kuwa hii chanjo sio salama, Msiwe na shaka, Chanjo hii ya Polio ni salama kabisa na haina madhara yoyote na sio mara ya kwanza kuwapatia watoto wetu, hakikisheni watoto wanapewa chanjo hii, na wazazi toeni taarifa kwa wazazi wenzenu ili kuokoa taifa letu la kesho" Amesema RC Shigela.
RC Shigela, amesema kuwa mambukizi ya virusi vya Polio ni maambukizi yanayoathiri mfumo wa Neva na huweza kusababisha udhaifi wa misuli au Kupooza, ambayo ni kushindwa kusogeza misuli.
Aidha, amesema kuwa Polio husambazwa kwa kugusana na mtu aliyeambukizwa,au kwa njia ya kinyesi chenye maambukizi.
Ikumbukwe kuwa Ugonjwa wa Polio huathiri zaidi Watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa sababu Kinga ya mwili yao iko chini. Dalili za ugonjwa huo ni Homa,mafua, maumivu ya mwili, kichwa na shingo au ulemavu wa ghafla wa viungo vya mwili.
"kumbuka Matone mawili ya chanjo ya Polio, Tanzania Bora Kesho" Okoa taifa la kesho kwa kupata chanjo" Ameongeza RC Shigela.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa