Manispaa ya Morogoro kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa umma kanda ya Mashariki wameanza kuzindua klabu za maadili kwa vijana wa shule za Msingi, sekondari na vyuo vikuu, ikiwa ni utekelezaji wa mikakati ya serikali kuweka misingi ya uadilifu kwa vijana tangu wakiwa wadogo kwa kuandaa wanafunzi watakao kuwa mabalozi wa kutoa elimu ya maadili.
Katika uzinduzi huo imeelezwa kuwa hali ya Uadilifu katika jamii hairidhishi, kutokana na kukithiri kwa mienendo iliyo kinyume na maadili ya kitanzania ikiwemo mavazi yasiyo kubarika,matumizi ya dawa za kulevya, pamoja na mimba za utotoni.
Uzinduzi huo unakuja ukilenga kuandaa vijana watakao kuwa mabalozi wa kueneza elimu ya maadili kuanzia ngazi ya familia na jamii inayo wazunguka, kutambua umuhimu wa maadili kwa taifa na athari zake pindi yakikiukwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi Ignas Sanga ambae ni afisa elimu sekondari Manispaa ya Morogoro anasema hatua hiyo itasaidia kuweka msingi wa vijana kujitambua na kupunguza wimbi la vijana wanaoishia kuwa watoto wa mitaani.
Aidha ameeleza uundwaji wa klabu hizo ni utekelezaji wa agizo la waziri wa TAMISEMI alilotoa Novemba 27 mkoani Dodoma katika maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu kuwataka wakurugenzi wa Miji na wilaya zote nchini kuratibu uundwaji wa klabu hizo kuanzia Shule za msingi hadi vyuo vikuu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa