WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema serikali inaendelea kudhibiti mianya inayowakwamisha wakulima wakiwemo wa uzalishaji wa mbegu za mafuta wenye lengo la kutosheleza mahitaji ya ndani.
Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizindua Maonesho ya Wakulima – Nane Nane ( Augosti mosi) katika Kanda ya Mashariki kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro.
Alisema kuwa, Serikali inaandaa mazingira mazuri yatakayomuwezesha mkulima kuzalisha mazao ya aina mbalimali kwa faida yakiwemo ya mbegu za mafuta ili kutosheleza mahitaji ya taifa.
Waziri Mwijage alisema , lengo ni kujenga uchumi shindani na imara kuelekea uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Pamoja na hayo , katika suala la uwekezaji Waziri huyo aliiagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), kuwapa ushauri wanafunzi wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) walioamua kuanzisha kiwanda cha maziwa -Shambani Milki .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe licha ya kuzungumzia mikakati ya mkoa katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara alisema viongozi wa kanda hiyo wamejipanga kuuboresha uwanja huo.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwahimiza wakulima kujikita katika suala la matumizi ya teknolojia za kilimo bora na ufugaji wa kisasa na jambo hilo kuwa agenda ya kudumu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa