Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kinatarajiakupanda miche ya miti aina mbalimbali ipatayo 53,000 kwa mwaka huu(2019),mkoani Morogoro ambayo ni hatua ya kukabiliana na athariya mabadiliko ya tabianchi, kuhifadhi mazingira na urejeshaji uotowa asili kwenye milima ya Uluguru.
Rasi wa Ndaki ya Misitu,Wanyamapori na Utalii wa ChuoKikuu hicho , Profesa John Kessy alisema hayo kabla ya KaimuMakamu Mkuu wa Chuo hicho , Profesa Peter Gillah,kumkaribisha KatibuTawala wa Mkoa wa Morogoro ,Clifford Tandari kuzindua wiki ya upandaji wa micheya miti SUA .
Profesa Kessy alisema ,tangu kampeni hiyo iliyoanzishwamwaka 1997, Chuo Kikuu hicho kimefanikiwa kupanda miche ya miti jumla yaekari 328 kwenye maeneo yanayokizunguka.
Alisema ,katika utekelezaji wa mpango mkakati huo , jumlaya miche ya miti 578,300 imepandwa maeneo mbalimbali ya mkoa huosambamba na kwenye vyanzo vya maji vya milima ya safu ya Uluguru naMindu .
“ Kwa mwaka huu wiki ya upandaji miche ya mitiSUA imepanga kupanda miti 22,000 na itakayobakia itagawiwa kwa wananchi nataasisi za umma na binafsi “ alisema Profesa Kessy.
Alisema ,tayari Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro imechukuamiche ya miti 500 kwa ajili ya kuwagawia wananchi wanaoishi safu ya milima yaUlunguru ili waweze kupanda na lengo ni kuhifadhimazingira , wakati Manispaa ya Morogoro pia imechukua miche 500.
Profesa Kessy alisema kuwa, Kauli mbiu ya Chuo Kikuu hichokwenye wiki ya upandaji miti mwaka huu ni : Panda miti kuimalishaeneo lako kuzuia migogoro ya Ardhi” .
Naye Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo kikuu hicho,Profesa Gillah alisema kuwa, shughuli za upandaji wa miti katikaChuo hicho ni endelevu.
Profesa Gillah ambaye ni Naibu Makamu Mkuu waChuo Taaluma alisema , upandaji wa miti n i sehemu yautekelezaji ulianza kufanyika tangu mwaka 1997 ambao lengo lake ni kuhifadhimazingira yanayoharibiwa na binadamu kutokana na shughulizao mbalimbali za kuzalisha mali.
Naye Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu hicho Utawala naFedha ,Profesa Fredirick Kahimba aliwataka wananchikujitokeza kuchukua miche hiyo kwa kuwa itatolewa bure kwaopamoja taasisi za umma , binafsi na shule za msingi na sekondarimkoani Morogoro .
Pamoja na hayo aliwataka wanafunzi wa Chuohicho kutumia wiki hiyo kujifunza kwa vitendo namna ya upandaji wamiche ya miti ili wamalizapo masomo yao wawwe nauweledi wa kuitumia elimu hiyo kwa manufaa ya watanzania .
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa ,Tandari aliwataka wadaumbalimbali na wananchi wa mkoa huo kuziunga mkono juhudi za Chuo Kikuu hichokwa kujitokeza kupanda miti kwa wingi katika maneo yao kwa lengo lakuhifadhi mazingira, kudhibiti migogoro ya mipaka na miti nibiashara.
“ Ombi langu kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro juhudi hiziza SUA ziendelea kuungwa mkono ili kuendelea kulinda mazingira yetu” alisemaTandari.
Hata hivyo aliutaka uongozi wa Chuo Kikuu hicho kuendeleana kutekeleza malengo yaliyoainishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius KambarageNyerere alipokizundua Chuo hicho.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa