KANISA la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) , Bethel Revival Temple, Mtaa wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro chini ya Mchungaji wake, Dkt. Barnabas Mtokambali wamekabidhi jumla ya Madawati 100 Shule ya Msingi Mwembesongo Kata ya MjiMpya.
Madawati hayo yamekabidhiwa Mei 09/2024 na kupokelewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, pamoja na Uongozi wa Kata ya MjiMpya wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Emmy Kiula.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Madawati hayo, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) , Bethel Revival Temple lililopo Mtaa wa Mwembesongo Manispaa ya Morogoro , Dkt. Barnabas Mtokambali ,amesema msaada huo ameutoa kutokana na ukaribu na ushirikiano mzuri wa Uongozi wa Kata hiyo na Uongozi wa Shule.
"Leo tumetatua changamoto ya watoto wetu,tuna historia na shule hii, kamwe kanisa letu hatuwezi kuisahau shule hii,nimekaa na wazee wangu wa Kanisa wakasema tuwape madawati 100 ili tumalize changamoto yao na leo tumetimza ahadi yetu "AmesemaDkt. Mtokambali.
Kwa upande wa Mstahiki Meya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, ameshukuru Kanisa la T.A.G kwa msaada wao wa Madawati 100 huku akisema kuwa msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani na hakuna mwanafunzi ambaye atakosa sehemu ya kukaa.
"Tunawashukuru wadau wetu, haya madawati watoto wetu wote watakaa kwenye nafasi zao, lakini hata waalimu unawapa nafasi nzuri ya kufundisha na wanafunzi wakaelewa vizurri darasani, milango ipo wazi Manispaa karibuni wadau kwa maoni, ushauri na misaada sisi kama Serikali tutaendelea kutoa ushirikiano" Amesema Kihanga.
Naye Diwani wa Kata ya Mji Mpya, Mhe.Emmy Kiula,amesema T.A.G wamekuwa msaada kwa Kata hiyo kwani wamekuwa wakiwa karibu na changamoto za wana Mji Mpya hususani Shule ya Msingi Mwembesongo.
“Niseme kutoka moyoni nimepata faraja kubwa kwa ndugu zetu kutukumbuka,wamekuwa msaada mkubwa sio tu kwenye madawati , bali wamekuwa wakitusaidia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Afya, Mazingira na huduma nyingine za kijamii. ,na hili pia la kutupa madawati ni tukio jema la faraja” Amesema Kiula
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa