Serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) imetoa jumla ya Tsh 16,740,000.00 kata ya Chamwino iliyopo ndani ya Manispaa ya morogoro na kunufaisha jumla ya kaya 512, ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini.
Fedha hizo zimetolewa na mratibu wa TASAF wa Halmashauri Bibi Felician Katemana ambaye amesemaa fedha hizo zitagawanywa kwa walengwa wa mpango huo, ambao ni wazee,vijana,wajane,wagane na kwa kaya maskini.
Aidha mratibu wa TASAF amefafanua kuwa kuna aina mbili za ruzuku inayotolewa, kwanza ni ruzuku ya msingi ambayo haina masharti na pili ni ruzuku ya masharti ambayo hutegemea aina ya familia.
Akizungumza na walengwa wa mpango huo Mstahiki Meya wa Manispaa ya morogoro Mhe. Paschal Kihanga amewasisitiza wananchi hao kuzitumia fedha hizo kwa matumizi sahihi na sio kuzinywea pombe.
Nae mwenyekiti wa mtaa wa tupendane Ndg Fransis Sentimali ametoa shukrani kwa uongozi na ameeleza kuwa baadhi ya walengwa fedha zao hupunguzwa kutokana na kutozingatia masharti, hivyo aliwasisitiza wananchi kutumia fedha kwa malengo sahihi na kuwahasa wananchi kushukuru kwa kidogo wanachokipata.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa