Ujenzi wa soko kuu litakalokuwa la kisasa katika Manispaa ya Morogoro unatarajia kuanza wakati wowote baada ya Serikali kuu kutenga kiasi cha Sh bilioni 10 za ujenzi huo katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , John Mgalula alisema hayo juzi wakati akijibu swali la papo kwa papo kutoka kwa Diwani wa Kata ya Sabasaba Mudhihir Shoo .
Diwani huyo alitaka kujua kinachokwamisha kuanza kwa ujenzi wa soko kuu la Morogoro baada ya kuvunjwa miaka miwili iliyopita kupisha kujengwa soko jipya la kisasa
Baraza la madiwani wa Manispaa hiyo lilifanya kikao chake cha kawaida chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga .
Kwa mujibu wa Mkurugenzi katika majibu yake ,alitoa ufafanuzi kuwa taratibu zote za kupata vibari zimekamilika na kwa sasa uchambuzi wa kumpata mkandarasi baada ya zabuni kutangazwa na kujitokeza wakandarasi wengi kuomba kazi hiyo.
Mgalula alisema , tayari Serikali kuu kupitia Mpango wa Kuimarisha Serikali za Mitaa Mijini (ULGSP) Mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) imeitengea Manispaa kiasi cha Sh bilioni 10 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa soko la kisasa.
“ Kwa sasa kazi ya wataalamu ni kufanya uchambuzi wa maombi ya wakandarasi na baada ya hapo jina litakaloshinda litawasilishwa kwenye Bodi na kamati ya fedha na baadaye kufikishwa kwenye baraza la madiwani kwa uamuzi wa mwisho” alisema Mgalula.
Alisema kuwa , bajeti ya mwaka wa fedha ya 2018/2019 inatarajia kuanza kutumika kuanzia Julai 2018 ni baada ya kikao cha Bunge kumalizika na kupitisha matumizi ya mwaka .
Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo, aliwapongeza madiwani na wafanyabiashara kuwa watulivu wakati wote wa mchakato wa awali kuwezesha kujengwa soko jipya la kisasa wakiwemo na viongozi wa serikali ya wilaya na mkoa hadi hatua ya upatikanaji wa fedha kutoka serikali kuu ya kujenga soko hilo.
Soko kuu lililokua linatumika kabla a kufunjwa mwazoni mwa Otoba mwaka 2016 lilikuwa limejengwa mwaka 1953 na wakoloni na lilikuwa ni chakavu kupindukia kutokana na kuzidiwa na uwepo wa idadi kubwa ya wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa