WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI), Angellah Kairuki amewaonya watumishi katika sekta ya elimu wanaodaiwa kutumia madaraka yao kwa kutoa vyeo kwa misingi ya Rushwa kuacha mara moja kabla hawajabainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Waziri Kairuki alisema hayo Januari 9, 2023 mjini Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha mapitio ya tathimini ya utekelezaji wa shughuli za uboreshaji na usimamizi wa elimu kwa mwaka 2022 na mpango mwaka 2023.
Waziri amesema wapo baadhi ya watumishi wa sekta ya elimu wanaodaiwa kutoa rushwa ili kupata madaraka ya Ofisa elimu wa wilaya na ngazi nyingine jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kiutumishi na ni kosa kisheria.
Kairuki amesema hategemei endapo mkuu wa shule amepata cheo hicho kwa kutoa rushwa kwani hataweza kufanya kazi kwa uadilifu, kwa maana lazima atafanya kila njia ili aweze kurejesha kile alichotoa.
" Nasema kama mambo haya yapo yakome mara moja, Serikali ipo makini, hatutawafumbia macho wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivi na kwamba wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria "amesema Waziri Kairuki
Waziri amesema kwa upande wa viongozi kuna nyakati wamepewa madaraka ya kukathimisha uongozi na kupendekeza wanaostahili kushika nafasi mbalimbali za uongozi na kuwataka kuwa macho.
“ Tumetoa mwongozo wa teuzi mbalimbali katika sekta yetu ya elimu katika mamlaka za Serikali za mitaa , ni vema tukafuata miongozo hiyo” amesema Waziri
Waziri amesema zipo tuhuma au yako maneno ya kwamba wengine wameingia kama maofisa elimu kwa kutoa rushwa , wapo wengine wamepata ukuu wa shule kwa kutoa fedha.
“Tutaendelea kuyangalia kwa umakini mkubwa,tunataka mtu anayepata nafasi ya uongozi awe ni yule kweli ni mahili yule anayekidhi vigezo vyote vilivyowekwa” amesema Kairuki
Pia amesema yako maneno ya kwamba wako baadhi ya maofisa elimu ili aweze kuteua baadhi ya wakuu wa shule ukipewa nafasi lazima watoe fedha na kila mwezi wanapekelewa fedha .
“ Kama yapo hayo kwa maofisa elimu yakome , kwa wakuu wa shule yakome na ikitokea wewe mkuu wa shule unashinikizo la kutoa fedha kwa yoyote …nitaancha namba zangu hapa tafadhari usisite kuweza kutoa taarifa na tutawalinda’ amesema Waziri
Waziri amesema Ofisi yake ipo macho na kwamba mabadiliko mengi yataendelea kufanyika na pia hatua zitachukuliwa za kisheria na hata za kijinai zitachukuliwa dhidi ya hao na kutoa rai kama wapo mambo hayo yakome.
Waziri pia amewatahadharisha watumishi wa umma wanaokiuka taratibu na kanuni za kiutumishi kwa kutoa lugha chafu kwa wananchi wanashungulikiwa kulingana na sheria za kinidhamu na kwamba itawekwa mitego kila sehemu zinapotolewa huduma za kijamii kwa watawatega kwa maswali ili mjibu lugha chafu tuwabaini wenye tabia za kutoa lugha chafu ili tuwachukulia hatua.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa