Wadau wa sekta ya Kilimo na Mifugo Manispaa ya Morogoro, wameupitia na kuujadili mpango wa kuendeleza sekta ya Kilimo Awamu ya pili katika kikao kilichofanyika tarehe 27/9/2019.
Akifungua kikao hicho Mwakilishi wa MKuu wa Wilaya ya Morogoro Ndg. Hilari Sagara, ameleza kuwa Manispaa ya Morogoro haina budi kukaa na kuweka mpango mkakati madhubuti utakaohakikisha kuwa, shughuli za Kilimo na Mifugo zinatekelezwa kwa tija ili kuongeza pato la mwananchi wa kawaida na kutoa uhakika wa usalama wa chakula na kuchangia katika Maendeleo ya Viwanda.
Aidha Ndg. Sagara alieleza kuwa awali sekta ya kilimo ilikuwa na Program ya kuendeleza Kilimo awamu ya kwanza (ASDP I), iliyoanza mwaka 2006/2007 hadi 20/3/2014. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuwepo kwa mfumo maalum wa kuandaa mipango ya Maendeleo ya Kilimo katika Wilaya (DADPS) kwa kushirikisha ngazi zote za Utawala, Upatikanaji wa vitendea kazi, Kuboreshwa kwa huduma za Utafiti na Ongezeko la Matumizi ya Pembejeo.
Sekta ya Kilimo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini sisi wadau kwa kushirikiana na sekta binafsi, tunayo nafasi kushiriki kikamilifu katika kuendeleza sekta ya Kilimo na Mifugo "Alisema Ndg. Sagara".
Serikali kwa kutambua mapungufu yaliyojitokeza katika program ya awali, imeamua kuandaa program ya miaka 10 (ASDP II) itakayotekelezwa katika awamu 2 ya miaka mitano-mitano. Program hiyo imeainishwa katika maeneo makuu 4 ikiwa ni pamoja na Usimamizi endelevu wa matumizi ya maji na ardhi, Kuongeza tija na faida katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi , Kuongeza tija na faida katika mazao ya Kilimo na Mifugo na Kuimarisha Uratibu, Ufuatiliaji na tathimini.
Nao wadau wa kikao hicho wameshauri wakulima kupewa elimu ya vifunganishio,matumizi sahihi ya mbegu,dawa na mbolea,usalama wa chakula.Aidha wakulima waliomba uwepo udhibiti wa wauza pembejeo feki,na kuishauri idara ya kilimo kufikiria kuanzisha bima kwaajili ya wakulima.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wawakilishi kutoka Shambani Milk,USAID The Future mboga na matunda,SUA,wadau wa Ngozi,SEED-CO,kituo cha ufugaji samaki Kingolwira na Benki ya NMB.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa