WANAWAKE Wajasiriamali Kata ya Kilakala wametakiwa kuongeza thamani ya bidhaa wanazozizalisha pamoja na kuboresha vifungashio ,ili kuhimili
ushindani wa soko la ndani na nje ya nchi.
Hayo yameelezwa na Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Morogoro anayetokana na Kata ya Kilakala, Mhe. Mwanaidi Ngulungu, katika kikao cha kuwachagua viongozi wa mpito na uundwaji wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Kilakala hivi karibuni.
Akizungumza na Wajasiriamali hao wakike, Mhe.Ngulungu, amesema kuwa bidhaa za wajasiliamali zinaweza kupata soko
kubwa iwapo zitaongezwa thamani na kufungashwa vizuri .
Mhe. Ngulungu, amesema kuwa baada ya Jukwaa hilo kuzinduliwa wataanzisha semina ya vikundi na wajasiriamali ili kuweza kuwapatia elimu
ya masoko na jinsi ya kupanga bajeti.
Kwa upande wa Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Kilakala, Delfina Pacho, amesema mchakato wa kuwapata viongozi wa kikatiba utafanyika baadae kwani kwa sasa wamefanya uchaguzi wa mpito ili kuweza kupata Jukwaa hilo la Wanawake Kata ya Kilakala.
Kwa upande wa Mjasiriamali maarufu Manispaa ya Morogoro, Lilian maarufu kwa jina la biashara Lilian Catering, anayejihusisha na usambazaji wa chakula, amempongeza Diwani Ngulungu kwa kuwakutanisha wanawake pamoja na kuahidi kushirikiana nao katika kufikia malengo yao.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa