Kituo cha Afya cha kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro , kinatarajiwa kukamilika hivi karibuni kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya Wananchi 30000 na Mitaa jirani.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo leo Julai 08/2022, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Dkt. Charles Mkumbachepa, amesema kuwa, Kituo hicho kinachogharimu jumla ya sh. Milioni 500 kinajengwa kupitia fedha za Tozo za huduma za simu ambapo kikikamilika kitaweza kuhudumia idadi hiyo ya watu na kuboresha huduma za afya.
Aidha, Dkt. Mkumbachepa,ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuhakikisha Wananchi wa Manispaa ya Morogoro wanapata huduma mbalimbali hususani huduma za afya pamoja na kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya afya na Zahanati ambapo kwa Manispaa ya Morogoro wamekamilisha Zahanati 6 na zote zimeanza kufanya kazi.
Mradi huo wa Kituo cha Afya cha Lukobe, ni miongoni mwa miradi itakayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 unaoongozwa na Kiongozi wa Mbio hizo 2022 , Ndug. Sahil Geraruma.
Mbali na huduma za afya, Dkt. Mkombachepa, amewaomba Wananchi wa Manispaa ya Morogoro kushiriki vyema katika SENSA ya Watu na Makazi itakayofanyika mwaka Agosti 23/2022 ambapo amesema huduma za afya zinazoendelea zitaimarishwa zaidi endapo Serikali watapa idadi nzuri ya Wananchi ili kuoboresha miundombinu na kuwaletea maendeleo.
“SENSA KWA MAENDELEO ,JIANDAE KUHESABIWA TAREHE 23/08/2022”
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa