Leo, tarehe 27.11.2023, Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Manispaa ya Morogoro, wamepatiwa mafunzo kwa vitendo, ya mfumo mpya wa kufanya tathimini ya kielektroniki, ya mahitaji ya rasilimali watu, itakayowezesha kila Divisheni na Kitengo kujua kama vinayo idadi kamili ya rasilimali watu wanaohitajika kulingana na majukumu ya Divisheni na Vitengo husika au kama kuna upungufu ushughulikiwe ili kuimarisha utendajikazi.
Mafunzo hayo yanayotazamiwa kumalizika kesho, yameendeshwa na wakufunzi kutoka Ofisi Rais Utumishi wakishirikiana na Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro.
Wajumbe wengine waliohudhuria katika mafunzo hayo ni pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya Morogoro, Kilosa na Mvomero.
MWISHO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa