Wafanyabiashara wadogo wa mkoa wa Morogoro na mikoa minginewamempongeza Rais , Dk John Magufuli kuwajali baada ya kuwaanzishia mfumowa kitambulisho cha mfanyabiashara mdogokwa gharama nafuu na kuwawezesha kufanya biasharamaeneo mbalimbali ya nchi kwa uhuru na bila kubughudhiwa.
Kiongozi wa Wafanyabiashara wadogo wa machinga wa mkoa,Faustine France alitoa pongezi hiyo kwa niaba ya wenzake na alisemakuwa hadi kufikia Februari 5, mwaka huu wafanyabiara wadogo 2,200 kati ya3,350 waliosajiliwa katika chama chao wamepata vitambulisho hivyo.
France alisema alitoa pongezi hizo na kusemahayo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, CliffordTandari wakati wa uzinduzi wa zoezi lakuwasajili na uuzaji wa vitambulisho hivyo kwenye viwanja vyabiashara vya Sabasaba vilivyopo Manispaa ya Morogoro .
‘ Tunampongeza Rais kwa kutupatia vitambulisho sisiwafanyabiashara wadogo ,na sasa tunaondokana na kubughuziwa na askari wa mgambowa Manispaa na watu wengine “ alisema France na kuongeza kuema .
“ Bado kama viongozi tunaendelea kufanya ufuatiliaji na piakuwasajiri wamachinga kwani kila mara idadi yao inaongezeka na lengo ni kupataidadi kamili na wanufaike na jambo hilo” alisisitiza France.
Kiongozi wa Wafanyabiashara wadogo alitumia fursahiyo kuwahimiza na kuwaomba wenzake “machinga” ndani yamkoa kujitokeza kwa wingi kuchukua vitambulisho kwa vile ni bei yakeni nafuu Sh 20,000 na kutumika kwa mwaka mzima.
Naye Meneja wa Soko la Sabasaba ,Joseph Makalla alisema,kuna viambata 480 ndani ya soko hilo na baada ya kukamilika zoezi hilouongozi wa soko utafanya uhakiki wa usajili wenyevitambulisho hivyo ,wenye leseni za biashara za Manispaa , nawaliopo kwenye mfumo wa VAT ili kubaini wale watakaokuwawanafanya biashara bila kufuata utaratibu.
Nao wafanyabiashara wadogo ,Sadiq Atanas pamojana Doto Adam wanaojishughulisha na biashara ya kuuza vinywaji baridistendi kuu ya Msamvu ,Manispaa ya Morogoro ambao ni miongoni walionunuavitambulisho hivyo kwa nyakati tofauti walisema kuwa watakuwa huru katikakufanya baiashara zao bila kusumbuliwa na askari wa mgambo.
“ Tumevisubiri kwa hamu vitambulisho hivi , wakati mkuu wawilaya na timu yake inahamasisha eneo la Msamvu , hatukuwa tumejipanga , lakinitulivyosikia matangazo leo zoezi lipo hapa Sabasaba tumekuja na nyaraka zetu natunafurahi tumevipata “ alisema Atanas.
Wafanyabiashara wengine walionufaika na mpango huo niwa kutoka mkoani Arusha ,Obeid Supuku pamoja na Kerika Laibon ambaowanajishughuliza na kuuza viatu kwa kutembeza mitaani wakisafiri mkoa mmojahadi mwingine na waliweza kukamilisha zoezi la kupata vitambulisho hivyo kwakutimiza masharti yaliyowekwa.
“ Binafsi mimi na wenzagu tunatoka Arusha hadi Morogoro namikoa mingine kuuza viatu na biadhaa nyingine , zoezi hili limenikutahapa Sabasaba kwa kuwa nina kitambulisho ya mpiga kura na picha ,nimejaza fomu na kupatiwa kitambulisho changu, nipo huru kwenda popote kuuzaviatu vyangu” alisema Laibon.
Katika awamu ya kwanza mkoa huo ulipokeavitambulisho 25,000 na kwenye kikao cha tathimini kilichoitishwa namkuu wa mkoa huo, Dk Kebwe Stepeh Kebwe Februari 4, mwaka huu ilionesha niasilimia 24 ya vitambulisho hiyo viliuzwa kwa walengwa .
Hata hivyo ,awamu ya pili mkoa umepatiwa vitambulisho40,000 ambapo mgawanyo wa kila halmashauri ambapo Manispaa yaMorogoro ikipatiwa 10,000 , nyingine idadi yake kwenye mabano Kilosa(7,000), Kilombero ( 5,000), Mvomero (5,000), halmashauri ya wilaya yaMorogoro(4,500), Gairo (3,500), Ulanga (2,500), naMalinyi (2,500) .
Mkuu wa mkoa aliwataka wakuu wa wilaya , wakurugenzi wahalmashauri kushirikiana kwa pamoja na wasaidizi wake kwenda maeneo ya walengwaili kutoa elimu na kuwaingiza katika mfumo wa kupata vitambulishohiyo na kutoa muda hadi Februari 28, mwaka huu zoezi liwe limekamilika .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa